UKRISTO WA KWELI
UKRISTO WA KWELI
SIFA KWA
UKRISTO WA KWELI
Wilberforce ni mmojawapo ya mashujaa wa kihistoria ya kisasa waliopuuzwa -hata Wakristo wengi hawajamfahamu Mkristo huyu shupavu wa fikra na pendo, ambaye mtazamo wake wa kibiblia, na utegemezi wa Roho wa Mungu, ulimpa moyo wa ujasiri, kuongoza juhudi za kumaliza utumwa.
Huyu ni mtu ambaye tunapaswa kusikia kutoka kwake , na Bob Beltz amefanya apatikane. Kitabu hiki, cha miaka 210 bado kinafaa sawia na umuhimu wake..
Kupitia kwa huu msaada wa Bob, ni jambo linalo inua moyo kukaa miguuni mwa Wilberforce, mtu ambaye Mungu alimtumia kubadilisha ulimwengu.
RANDY ALCON
MWANDISHI, HEAVEN AND SAFELY HOME
Tuseme ni kumaliza vizuri! Siku chache kabla ya kifo chake, juhudi za Wilberforce kumaliza utumwa huko Uingereza ziliendeshwa kwa mafanikio. Usiku ule wa toleo la picha ya kushangaza, ya Amazing Grace, kulikua na toleo jipya la filamu ya kitabu cha Wilberforce, Real Christianity, iliosahihishwa na kusasishwa na rafiki yangu Bob Beltz, ambaye pia alifanya kazi kwenye filamu hio. Ilikua ni zawadi nzuri sana ya Krismasi ya mwaka 2006 kwetu sisi sote!
BOB BUFORD
MWANZILISHI, LEADERSHIP NETWORK
MWANDISHI, HALFTIME AND FINISHING WELL.
Hiki ni kitabu ambacho nakipendekeza sana. Bob Beltz amefanya tafsiri ya kisasa kabisa ya mojawapo ya vitabu kuu sana ya Ukristo wa nyakati zote. Nimesoma na kurudia Real Christianity, yaani, Ukristo wa kweli, na nimepata ujumbe wake unafaa leo hata na vile ilivyokuwa wakati wa huyo kiongozi mkuu wa Kikristo, aliyekielelezo maishani mwangu, yaani William Wilberforce, alipoiandika. Usichukue kitabu hiki tu- lakini ukisome.
CHUCK COLSON
MWANZILISHI NA MWENYEKITI, PRISON FELLOWSHIP
Pengo kati ya imani ya kweli na Ukristo wa kidersturi ni pana leo kama ilivyokuwa wakati wowote katika historia, kwa hivyo kuna mengi tunaweza kujifunza kutoka kwa uamsho-na mafanikio ya kilio cha William Wilberforce. Bob Beltz ametufanyia huduma nzuri katika kufanya kitabu cha aina hii kinachouzwa vizuri zaidi kupatikana tena.
OS GUINNESS
MWANDISHI, UNSPEAKABLE FACING UP TO THE CHALLENGE OF EVIL
Mamilioni ya maisha yalibadilishwa kwa sababu ya uamuzi wa William Wilberforce kubadili jamii ya siku zake. Miaka mia mbili baadaye, mahitaji karibu yetu bado ni makubwa. Natumai watu wengi watasoma toleo hili jipya la kitabu cha zamani cha Wilberforce na kutiwa moyo na mfano wake.
NICKY GUMBEL
MWANDISHI, QUESTIONS OF LIFE AND A LIFE WORTH LIVING
Real Christianity ni juu ya kuishi alivyoishi Yesu, na kufanya vile Yesu alivyofanya. Lazima isomwe na kila mtu anayetaka kuishi maisha yake yote kwa Kristo tu.
WALT KALLESTAD
MHUDUMU MKUU, COMMUNITY CHURCH OF JOY GLENDALE, ARIZONA
Kwa muda mrefu Wilberforce amekuwa shujaa kwa wengi wetu. Sasa, kupitia Real Christianity, tunapata mtazamo mzuri katika theolojia yake, hali yake ya kiroho na shauku yake. Kwa kutumia kazi ya Bwana Wilberforce katika asili yake, Bwana Bob Beltz anatupa changamoto inayohitajika kwetu sote, kwa sababu sote mara kwa mara tunajaribiwa kupoesha imani yetu iliomoto ikawa vuguvugu na ya Ukristo wa kawaida.
BRIAN MCLAREN
MWANDISHI/ MWANAHARAKATI (BRIAN MCLAREN.NET)
Kitabu cha kihistoria, kinachobadilisha utamaduni kilichoandikwa na mwanasiasa mwiinjilisti aliyebadilisha historia ya Dola ya Uingereza. Kitabu hiki bado kinafaa hata leo.
RONALD J. SIDER
RAIS, EVANGELICALS FOR SOCIAL ACTION
UKRISTO
WA
KWELI
Falisi katika Kiingereza ya kisasa ya Mtazamo wa Vitendo wa Mfumo wa Kidini uliopo wa Wanaodai kuwa Wakristo wa Tabaka la Juu na la Kati katika nchi hii Ukilinganishwa na Ukristo wa kweli
Iliyochapishwa mnamo 1797
Kimeandikwa Na William Wilberforce, Esq.
Mbunge wa Kaunti ya York
Iliyorekebishwa na Kusasishwa na Dk Bob Beltz
YALIYOMO
Utangulizi wa Toleo hili ……………………………………………………….6
Na Dr Bob Beltz
William Wilberforce Mtu wa Msimu Wote ……………………… ... ………. 9
Na Kevin Belmonte
Utangulizi Asili wa Wilberforce ................................................................. 16
Sura ya Kwanza ……………………………………….……………………… 19
Hali ya Ukristo wa kisasa
Sura ya Pili ……………………………………………………………..……… 27
Mawazo ya Kisasa Kuhusu Asili ya Mwanadamu
Sura ya Tatu ……………………………………………………………………..41
Kuelewa Ukristo wa Kidersturi
Sura ya Nne ………………………………………………………………….…..63
Vigezo vya Kweli vya Tabia ya Kikristo
Sura ya tano …………………………………………………………………… 131
Hoja za Ukristo wa kweli
Sura ya Sita ..........................................................................................................139
Hali ya Kisasa ya Ukristo
Sura ya Saba ………………….. ………………………………………………...165
Vidokezo vya Kimsingi Kuhusu Imani halisi
Maandishi yaliyopendekezwa ……………………………………………………201
Yaliyokusanywa na Kevin Belmonte
UTANGULIZI WA HABARI HII
Dk Bob Beltz
Katika kurasa zifuatazo nitakutambulisha kwa kitabu cha kipekee na mojawapo ya takwimu za kushangaza katika historia ya Uingereza. Jina lake lilikuwa William Wilberforce. Labda unasoma kitabu hiki kwa sababu tayari umemjua mtu huyo lakini haujawahi kusoma maandishi yake. Kwa kweli ndivyo nilivyokuwa katika uzoefu wangu mwenyewe. Halafu, miaka kadhaa iliyopita, nilikuwa na bahati nzuri ya kuwa sehemu ya timu ambayo ilianza kutengeneza filamu ya Amazing Grace, ambayo ilitokana na maisha ya William Wilberforce.
Mwanzoni mwa mchakato wa kufanya kazi kwenye filamu hii niliamua kusoma toleo la kawaida la kazi ya asili ya Wilberforce juu ya imani ya Kikristo.
Jinsi unavyoweza kuona kwenye ukurasa wa anwani ya kitabu hichi, hii ilikuwa ni kazi iliyoandikwa wakati wachapishaji waliamini kwamba inampasa mtu kutoa habari nyingi iwezekanavyo katika kichwa cha kitabu chake. Mnamo 1797, mwaka ambao kitabu hiki kilichapishwa kwa mara ya kwanza, majina ya kuvutia hayakuwekwa wazi. Tangu wakati huo nimeona mara nyingi mada zikipunguzwa na hatimaye kuwa A Practical View of Real Christianity. Ila kusudi na lengo la BwanaWilberforce zilibakia. Kwa kazi yake, Bwana Wilberforce aliwalenga watu wa kundi la aina Fulani; kama watu walioishi kwa wakati fulani, na mahali fulani, ama watu walioshikilia mfumo wa aina fulani wa imani, hasa mfumo uliozalisha uzoefu maalum wa kidini. Kwa hivyo, ili kuunda mada sahihi na kamilifu kwa kitabu chake, Bwana Wilberforce mwenyewe aliandika kwamba maandishi yake yalikusudiwa kuwa Maoni juu ya Mfumo wa Kidini Unaojulikana, wa wale wanaojiita Wakristo -sio wa kundi lolote la watu wanaojidai kuwa ni Wakristo, bali ni wale wanaojiita Wakristo ambao wako kwenye Matabaka ya Juu na ya Kati katika Nchi hii (yaani Uingereza mnamo 1797). Ilikuwa ni aina hio ya mfumo wa imani ya kundi hili maalum, ndio iliwatofautisha na kundi lile ambalo Bwana Wilberforce aliliita “Ukristo wa kweli”- yaani Real Christianity.
Kwa sababu ya umaarufu wa kitabu hiki, ni ngumu kuthamini kabisa kazi iliyopo bila kumfahamu mwandishi na ulimwengu wa wakati wake. Sio nia yangu hata kidogo katika chapisho hii kuandika biografia ya William Wilberforce. Wale waliohitimu zaidi kufanya hivyo tayari wamekwishafanya kazi hiyo. Labda nikuelekeze tu kwa sehemu inayofuata, ambapo wasifu mfupi wa kumbukumbu ya shujaa wa ubinadamu (Hero for Humanity) wa Kevin Belmonte imejumuishwa, pamoja na orodha za nakala, ilioundwa kwa ustadi na Belmonte.
Kusudi langu katika kitabu hiki ni "kutafsiri" kazi ya Wilberforce kutoka kwa lugha ya mwisho ya karne ya kumi na nane kuwa kitabu kinachofikisha ujumbe wa Wilberforce kwa watu wa karne ya ishirini. Wabishi wa Wilberforce watapungua, nina hakika.
Lakini kwa wale wanaofanya hivyo, ikumbukwe kwamba Wilberforce, katika kitabu chake, alipendekeza kufanya hivyo hasa na vitendo kutoka kwa vizazi vilivyopita ambavyo havikuweza kufikiwa na watu wa kawaida kwa sababu ya lugha au mtindo wa uandishi. Kwa mfano, katika Sura ya 6 ya toleo la 1824 la A Practical View, Wilberforce hufanya maoni yafuatayo akizungumzia seti ya vitabu vya 1707 vilivyoandikwa na mchungaji wa Presbyterian Richard Baxter:
Toleo la 1707 la Practical Works la Baxter ni hazina ya hekima ya Kikristo, na itakuwa huduma muhimu sana kwa wanadamu kuirekebisha, na labda kuifundisha, ili kuipa ladha inayofaa zaidi kwa wasomaji wa kisasa.
Matumaini yangu na nia yangu ya kurekebisha na kusasisha kitabu hiki ni kwamba kizazi kipya cha wasomaji wa kisasa kitagundua huyu mtu wa ajabu na ujumbe aliouwasilisha.
Kabla ya kuendelea na utangulizi wa Wilberforce mwenyewe, wacha nikuambie kwamba nilifanya kazi kutoka toleo la kumi na tano la maandishi kamili A Practical View of Real Christianity. Toleo hili, lililochapishwa huko London na T. Cadell mnamo 1824, linatambuliwa kama toleo la mwisho la kitabu kilichohaririwa na Wilberforce mwenyewe. Ukurasa wa kichwa wa toleo hili una nukuu mbili chini ya kichwa chake cha muda mrefu. Nitaziwasilisha hapa kama zilivyoonekana kwenye ukurasa halisi:
Tafuta maandiko haya!-----
Yohana 5:39.
Ni jinsi gani FALSAFA YA KIUNGU inavyopendeza!
Sio kali wala haichoshi, kama wapumbavu wanavyodhani,
Lakini ni kama sauti ya kinanda ya Apollo,
Na kama kusherehekea peremende isioisha
Bila ukwasi wowote.
John Milton
Wilberforce alijua kuwa wasomaji wake wangefanya vizuri kufuata agizo la John ili kupata thawabu iliyoonyeshwa na Milton. Natumai toleo hili la kisasa la kazi ya Wilberforce litakuwa na athari wa namna hio.
WILLIAM WILBERFORCE:
MTU WA MAJIRA YOTE
Kevin Belmonte
Kwa kiwangoo yoyote, William Wilberforce alikuwa mtu wa kushangaza sana na kwa kweli ameelezewa kama "Mwana mageuzi mkubwa zaidi katika historia" 1. Urithi wake uliathiri maisha ya wengi wakiwemo wafalme pamoja na marais, na vile vile kugusa maskini na hata wanyonge katika mataifa mbali mbali ulimwenguni.
Wilberforce alizaliwa katika mji wa bandari wa Hull, Uingereza, mnamo Agosti 24, 1759, katika familia iliyofanikiwa, familia ya wafanyabiashara ambao leo tungewataja kama "tabaka la katikati". Familia yake ilikuwa na matumaini kwamba William huyu chipukizi angeongeza utajiri wa familia au labda angeshinda nafasi ya kifahari katika uchaguzi wa kisiasa. Matumaini haya hayakukosea. Miezi chache tu baada ya kuhitimu kutoka Chuo Kikuu cha St John's, Chuoni Cambridge mnamo 1780, Wilberforce alipewa kiti katika House of Commons kama Mbunge wa Hull- siku chache tu baada ya yeye kusherehekea mwaka wake wa ishirini na moja tangu kuzaliwa.
Kufikia wakati huu, Wilberforce alikuwa karibu na William Pitt the Younger, ambaye angekuwa Waziri Mkuu ambaye ni kijana zaidi katika historia ya Uingereza. Hawa vijana wote wawili walikuwa na vipawa kubwa vya kisiasa. Wilberforce alikuwa mjanja, mzuri na mwenye akili. Alikuwa na haiba ya kuvutia na aliimba vizuri hivi kwamba mnamo 1782, Mkuu wa Wales alisema atakwenda popote ili kumsikiza Wilberforce akiimba. Pitt, mwenyewe, mmoja wa wasemaji wakuu wa Uingereza, alisema kwamba Wilberforce ana ueledi wa usemi zaidi ya mtu yeyote yule amewahi kumjua. Vipawa hivyo vilimwezesha Bwana Wilberforce kushinda ubaguzi wa kitabaka uliowekwa na wasomi wakubwa (ambao walitawala Uingereza sana wakati huo) dhidi ya kundi la wafanyabiashara. Alikuwa kijana anayeinuka.
Pitt akapanda kuwa Waziri Mkuu mnamo 1783 akiwa na umri wa ajabu wa miaka 24. Na chini ya miezi sita baadaye, Wilberforce akachaguliwa kuwa Mbunge wa kaunti ya Yorkshire- mojawapo ya viti vyenye nguvu zaidi katika Baraza la Commons. Ila njia ya Wilberforce ikachukua mkondo tofauti sana na ya Pitt kufuata uchaguzi wake. Huku akitamani kufurahia mafanikio yake kisiasa, Wilberforce alianza safari ya kwenda Ulaya na familia yake na marafiki wachache waalikwa. Baada ya miezi kadhaa, alirudi huku moyo wake ukiwa katika lindi la mahangaiko lilikolea kutokana na mazungumzo aliyokuwa nayo na Bwana Isaac Milner, mmoja wa wale wenzake waliosafiri naye. Milner, Mwanglikana Mwiinjilisti, alikuwa Mtu wa Jumuiya ya Royal Society (taasisi ya kitaifa ya Sayansi ya Uingereza) na baadaye rais wa Chuo cha Malkia huko Cambridge. Kwa ueledi wake wa ufafanuzi alikua amemwelezea Bwana Wilberforce juu ya "moyo wa marifa ya Kikristo" 2
Wilberforce alirudi London mnamo msimu wa 1785, huku amejawa na mashaka juu ya hatima yake. Mazungumzo yake na Milner yalikuwa yamemshawishi kuhusu ukweli wa Ukristo, lakini hakuona jinsi, au ikiwa, Mkristo anaweza kumtumikia Mungu katika siasa. Alikuwa katikati ya kile angeelezea baadaye kama "Mabadiliko Makubwa", au kushikilia Ukristo wa Kiinjilisti.
Pasi na kujua mahala pengine pa kugeukia, Wilberforce alimtafuta John Newton, nahodha wa zamani wa meli ya watumwa aliyegeuka mhudumu wa Kinglikana ambaye tunamkumbuka leo kama mwandishi wa wimbo wa "Neema ya Ajabu" yaani Amazing Grace. Wilberforce alikuwa amemjua Newton akiwa bado mvulana mdogo tu. Lakini familia ya Wilberforce ilishtushwa na ushirikiano wake mkubwa na mtu ambaye walimwona kama mtu shupavu wa dini; hiyo wakamtenga na ushawishi wa Newton na ya mjomba na shangazi yake mwinjilisti ambao Wilberforce alikuwa akikaa nao.
Walakini mbegu nzuri iliyopandwa ndani ya moyo wa Wilberforce na Newton (na mjomba na shangazi yake) haikunyauka kabisa. Iwapo Wilberforce angemhitaji mtu wa kumkimbilia, bila shaka alijua anafaa kumtafuta Newton. Alikuwa ndiye chaguo anayemfaa.
Newton alisaidia Wilberforce kuona kwamba Mungu alikuwa na kusudi maalum katika maisha yake- kwamba anaweza kumtumikia Mungu katika siasa na kufanya mabadiliko huko, kama vile Danieli na Yosefu wavyofanya katika nyakati za Agano la Kale. Kufikia 1787, Wilberforce alikuwa ameshikilia jukumu ambalo kwalo leo hii tunamkumbuka: vita vya kumaliza biashara ya watumwa wa Uingereza. Na ilikuwa ni John Newton, mfanyabiashara wa zamani wa watumwa, ndiye Mungu alimtumia kumsaidia Wilberforce kuona kwamba mwelekeo huu ndio inampasa kuchukua. Si ni kinaya kwamba mtu aliyekua na makosa ya jinai dhidi ya binadamu hivi leo amegeuka na anamfundisha rafiki yake njia bora ya kuwahudumia na kuwasadia wanadamu!
Wakati huo huo, Wilberforce alijitoa kimasomaso kuhamasisha mabadiliko katika ukuzaji wa maadili na dersturi huko Uingereza. Kama alivyoandika katika shajara yake mnamo Oktoba 28, 17 87, Mungu alikuwa ameweka vitu viwili vikubwa mbele yake: kukandamiza biashara ya watumwa na kazi ya mageuzi ya maadili. Na kwa hiyo, hata na alipokua akipigana vita vya kumaliza biashara ya watumwa huko Uingereza, (vita vilivyomchukua miaka 20 kumaliza), Wilberforce alianza hatua nyingi za mipango ya uhisani. Katika mjadala wake na wahabari wenzake katika Clapham circle (waliitwa hivyo kwa sababu waliishi karibu sana mmoja kwa mwingine katika kijiji cha Clapham), alifuatilia marekebisho ya kila aina.
Wilberforce aliongoza au alikuwa mwanachama wa angalau jamii 69 nzuri. Alikuwa mwanzilishi na mchangiaji wa magazeti kama Christian Observer, Christianity today yaani Ukristo Leo wa wakati wake. Alisaidia kuanzisha eneo la kikoloni huko Sierra Leone kwa watumwa walioachiliwa, Jumuiya ya Kifalme ya Kuzuia Ukatili kwa wanyama, hospitali za maskini, Taasisi ya Kifalme ya Uingereza (iliyowekwa wakfu kwa utafiti wa kisayansi), na Jumba la Sanaa la Kitaifa. Alikuwa pia mwanaharakati wa mageuzi ya kielimu, mageuzi ya magereza, ukuzaji wa mipango ya afya ya umma na kutetea masaa mafupi ya kazi na hali zilizoboreshwa katika tasnia.
Wilberforce aliwahifanya kazi na watu wengi waliokuwa na mitazamo tofauti na yake kuhusu ulimwengu wa Kikristo, lakini kila siku juhudi zake zilikuwa ni kuwa chumvi na nuru kwa watu wake. Kazi yake, wakiwa na Bwana Jeremi Bentham, ya mageuzi ya magereza ni mojawapo ya mifano hio, na ushirikiano wake na Bwana Charles Fox katika kukomesha biashara ya watumwa ni mwingine. Wilberforce aliamini kwamba, "Ni jukumu la kimsingi la kila mtu kudumisha furaha ya wenzake kadri awezavyo."3
Mojawapo ya mambo Wilberforce alidumisha kama desturi yake ilikuwa ni uchapishaji wa kitabu chake A Practical View of the Prevailing Religious System… Contrusted with Real Christianity mnamo 1797. Kiliweza kuuzwa kwa haraka sana na hata toleo nyingine tano zikatolewa kwa muda wa miezi sita. Kufikia 1826, matoleo 15 yalikuwa yamechapishwa huko Uingereza, na matoleo 25 yalikuwa yamechapishwa huko Marekani. Kilitafsiriwa kwa Kiholanzi, Kifaransa, Kijerumani, Kiitaliano na Kihispania.
Maoni ya kweli juu ya Ukristo wa kweli iligusa maisha ya wengi kote Uingereza. Edmund Burke, mtaalamu mkubwa wa siasa na mpatanishi, alikuwa amekisoma kitabu hiki siku chache za mwisho za maisha yake na akafarijika sana, hata akatuma ujumbe kwa Wilberforce akisema kwamba iwapo angeishi, angemshukuru sana rafiki yake huyo kwa "kutuma kitabu kama hicho ulimwenguni" .4 Kitabu hiki kilisaidia sana katika kubamdilisha mwanafalsafa wa maadili wa Scotland Thomas Chalmers, pamoja na mwandishi maarufu wa mambo ya kilimo na safari Arthur Young.
Kwa watu wa wakati wa Wilberforce, kitabu, A Peactical View of Real Christianity kilikuwa ni ombi (kilio kutoka moyoni ") kwa Waingereza wenzake kukumbatia kile alichokiita kuwa Ukristo kamili au halisi. Tofauti na vitabu vingi vilivyochapishwa kwa wakati huu, A Practical View of Real Christianity kilikuwa kitabu cha kupendeza na cha kutajika. Kilikuwa tamko la dhamira ya imani ya Wilberforce, na kwa hivyo, hakikuonyesha tu ushawishi wa Jonathan Edward na Philip Doddridge, bali pia kiliweka mbele maono ya Wilberforce ya jamii nzuri. Wilberforce aliamini kwamba watu ambao maisha yao yamebadilishwa na kweli za Kikristo wangeweza kuongeza thamani ya jamii ambamo walikuwa wakiishi. Na kama urithi wake unavyoshuhudia, alikuwa sahihi.
Kwa sababu ya afya mbaya, Wilberforce alistaafu kutoka kwa maisha ya kisiasa mnamo Februari 1825, akiwa ametumikia taifa lake kwa takribani miaka 45, lakini shauku yake ya kupata dhamana ya watumwa kwa makoloni yote ya Uingereza iliendelea bila kufifia. Alishiriki katika kusukuma maombi, na kuwaelekeza wanasiasa wachanga (kama vile Sir Thomas Fowell Buxton na Lord Shaftesbury) ambao walirithi vazi lake, na pia alijitahidi kuhutubuia uma iwapo kuliwezekana. Siku tatu kabla hajafa, alijulishwa kwamba Bunge lilinuia kupitisha sheria ya kumaliza utumwa katika Milki yote ya Uingereza.
Kati ya Wamarekani-Waafrika wengi ambao maisha yao yalishawishiwa na Wilberforce walikuwapo William Wells Brown, Paul Cuffe na Fredric Douglas. Mababa wengi wanzilishi wa Merekani pia walishawishiwa na kazi ya Wilberforce, pamoja na John Quincy Adams, John Jay, Thomas Jefferson, Rufus King, Marquis de Lafayette na James Monroe. William Hooper, mwimbaji wa Tangazo la Uhuru, hata alimpa mwanawe jina William Wilberforce Hooper.
Kati ya wanafasihi walioathiriwa na Wilberforce walikuwemo Thoreau, Emerson na Whittier. Jedidiah Morse ("baba wa Jiografia ya Marekani") alimhesabu Wilberforce kama rafiki, vile tu mwanawe Samuel Morse- msanii na mvumbuzi alivyofanya; alimhesabu Wilberforce kama "Leonardo da Vinci wa Marekani." Mianga mingine wa tamaduni ya Marekani ambayo maisha yao yaliguswa na Wilberforce ni pamoja na Caspar Morris, Lyman Beecher, Harriet Beecher Stowe, William Lloyd Garrison, Edward Everett, Jonathan Edward, Jr., Timothy Dwight (Rais wa Yale), William Jay, George Ticknor, Abraham Lincoln, William Buell Sprague, Charles Sumner, William Cabell Mito, EM Bound, Arthur na Lewis Tappan, Henry Ingersoll Bowditch, na wazazi wa mshairi mwenye ueledi wake Wilberforce Lord.
Ushawishi wa Wilberforce (na mduara wa Clapham) bado haujakamilika. Chuo kikuu cha Wilberforce cha Ohio, chuo kongwe cha zamani zaidi cha Wafrika- Wamarekani, kinaendelea kuelimisha vijana katika siku zetu. Viongozi wa Kidemokrasia na Republican katika Nyumba na Seneti wanaendelea kupata msukumo kutoka kwa urithi wa Wilberforce. Ushirika wa Magereza, Jukwaa la Wilberforce na vikundi vya Baraza la Utatu vinamuheshimu na kukuza jitihada zake katika utamaduni mpya. Kwa kweli kazi ya Wilberforce haijamalizika.
Kufuatia kustaafu kwa Wilberforce mnamo 1825, Robert Southey, Malenga gwiji wa shairi wa Uingereza kutoka 1813 hadi 1843, alilipa ushuru kwa huyu rafiki yake wa zamani. Maneno ya Southey hutumika sawa na ushuru kwa urithi wa kudumu wa Wilberforce: Southey aliandika, Nyumba ya Commons "haitaweza kuona kama wewe tena" .5
Kumbuka
UTANGULIZI HALISI WA WILBERFORCE
Utetezi wa mwandishi: Ninachojaribu kutimiza
Imekuwa hamu yangu kwa miaka mingi kuwaandikia wananchi wenzangu juu ya imani.1 Sikuweza kufanya hivyo hadi sasa kwa sababu ya shughuli zinazoambatana na wadhifa wangu kisiasa na pia hali ya afya yangu duni. Kwa muda mrefu nimekuwa nikitarajia uwezekano wa kupata msimu fulani usio na shughuli nyingi, ambao utaniwezesha kuweka umakinifu wangu wote katika kazi hii. Nilikuwa natazamia wakati ambapo sisumbuliwi na mambo mengine, ili kwa juhudi na umakinifu niweze kuandika kwa njia ambayo msomaji hatatiziki na kazi yangu. Mwishowe ikawa dhahiri kwangu kwamba msimu kama huo hatimaye umepatikana. Kwa hivyo, nimechukua nafasi hii ya bure ili nitekeleze kusudi nililotumainia. Kwa hivyo, niwie radhi kwa kosa lolote linalotokana na mbinu ya uandishi.
Bila kuzingatia hisia yako msomaji kuhusu ubora wa uandishi, wacha nikuhakikishie kwamba kile nimeandika katika kurasa hizi hazijaafikiwa bila uangalifu mkubwa. Nafahamu kwamba anwani ya kitabu ni muhimu sana, hivyo nimeitafuta kwa uangalifu mkubwa, na kwa kujihoji na kukariri mara kadhaa yote utakayoyasoma.
Bila shaka mtu anaweza kutoa pingamizi kwamba kwa vile mimi sio mwanatheolojia, sistahili kushughulikia suala hili. Ikiwa yanipasa kujitetea dhidi ya pingamizi hilo, basi naweza kusema kwamba waandishi wengine tayari wamekwishafanya vivyo hivyo. Lakini nadhani sote tuna jukumu moja la kujitahidi kimasomaso ili kukuza ustawi wa wenzetu. Kwa mfano, iwapo wampenda mtu ila yaonekana wazi kwamba hauna nia njema na maisha yake, kwa kumhangaisha, ilhali, ni mnyonge, na hawezi fanya lolote kujitetea, ama labda anaogopa vile watu watakayomwona; basi ijulikane wazi kwamba wewe humpendi, bali unamtumia tu kwa ukatili wako; ama kweli, hauna moyo.
Napenda kupendekeza kwamba imani ni jukumu la kila mtu kwa sababu shughuli za imani zinamshikamano mkubwa sana na ustawi wa kijamii kiasi cha kwamba haifai mwanasiasa kuzipuuza. Kwa kuongezea, ukweli kwamba mimi si kuhani wala mhudumu kanisani waweza kusaidia watu kuona wazi zaidi yale yanayosemwa katika kitabu hiki. Kwa hivyo, hakuna mtu anayeweza kunishtaki kwa kuandika kile ninachokiandika kwa msingi ya kuwa nimevutiwa na ubinafsi kama kuhani au chuki ya kitheolojia.
Haya basi, nimekwisha toa tetezi na mahalalisho za kutosha; sasa wacha niendelee na kazi hii kuu sana ninayo, kwa maana ndio madhumuni yangu kuu katika kuandika kitabu hiki.
Sitajaribu kuwashawishi wakosomaji au kujibu maswali ambayo yaonekana wasioamini huuliza, lakini badala yake nitaeleza baadhi ya shida za waumini na vitendo vya wale ambao tayari wanadai kuwa ni Wakristo. Hapa najaribu kulinganisha kile tunachokiona kwenye maisha ya wengi, (labda wengi, ambao hufanya madai haya), na yale ninaelewa Bibilia inafundisha juu ya maana halisi ya kuamini katika Kristo. Ninasikitishwa ninapoona wengi wa wanaojiita Wakristo wakiwa na uelevu mdogo sana juu ya hali halisi ya imani wanayoidai. Imani ni somo lenye umuhimu sana; hivyo basi hatufai kuipuuza kwa ajili ya uvuto au usumbufu wa maisha haya. Yatupasa kuelewa kwamba sote tutatoa hesabu mbele za Mungu kwa jinsi tulivyoishi maisha yetu. Nami sitoi tisho lolote kwa kuandika juu ya ukweli huu. Natumai utayatia manani yale niliyonakili katika kurasa hizi.
Haya! Ndio yote naweza sema kwa utangulizi. Ikiwa yale ninayoandika yanaonekana kuwa ngumu sana kwako, nitakuuliza tu ukayaangalie ninayoyasema dhidi ya yale ambayo Biblia inafundisha. Hayo ni maoni tu ambayo ni muhimu. Ukikubali mamlaka ya Bibilia, nadhani utayakubali.

- Maelezo yaliyotolewa katika hotuba ya Dk. Os Guiness, Mkufunzi wa Kikristo, mwandishi na msemaji.
- J. Pollock, Wilberforce (London: John Constable, 1977), P.34
- W. Wilberforce, A Practical View of Christianity, ed. Kevin Belmonte (Peabody, M.A: Hendrickson Publisher, 1996), n.p.
- Kevin Belmonte, “William Wilberforce: The Making of an Evangelical Reformer” (master’s thesis, Gordon-Conwell Theological Seminary, 1995), p.2
- Robert Isaac and Samuel Wilberforce, The Life of William Wilberforce, vol. 5 (London: John Murray, 1838), p. 238