Kuweka Moyo mbele ya Farasi.
Kuweka Moyo mbele ya Farasi.
Hivi majuzi, tumepokea baraka pasinakipimo katika usomaji wa kitabu "Ukristo wa kweli". Kitabu hiki kiliandikwa na William Wilberforce. Huenda baadhi yenu mmekwishasikia jina hili na mnamjua kama nguvu zilizoongoza katika kukomesha utumwa huko England, hapo nyuma mwishoni mwa karne ya 18 na mapema karne ya 19 - akimtanguliza Mchungaji kwa karibu miaka 50.
"Ndugu au dada katika Ukweli anaweza kupata imani ya Mkristo" aliye wa kawaida "kwa njia fulani kuwa inachukiza au sio halisi. Lakini iwapo tutachukua wakati na kumjua yule anayeitwa “mwamini wa kawaida”, inaweza kutushangaza kugundua namna ana usafi wa moyo ambao itatutia aibu sisi wenyewe. Katika hali nyingi, kile tutakaopata ndani yao ni ishara wazi ya Roho Mtakatifu akifanya kazi mioyoni mwao na maisha yao, pamoja na upendo wa Kristo, bidii na bidii katika kazi yake Kristo, busara, upole na utulivu . Tabia kama hizo hazihitaji hoja ya kutetea. "
Ndugu, mpinzani wetu asiye tulia, asiye legea, asiye na huruma, mpinzani asiye choka -yaani Shetani, Ibilisi, Lusifa - anatafuta kutuangamiza. Ana mishale isiohesabika katika podo lake kukamilisha kazi yake ile moja tu, kutuhusu – sisi wazaliwa wa Roho. Kwa vurugu zote anazozijua, hutafuta kuzimisha nuru ya ulimwengu. Na wakati mwingine, bila hata kujua, tunaweza kujikuta tukimsaidia - haswa kama inavyohusiana na mgawanyiko na usemi mbaya. Tukikumbwa na mabmo kama hayo, mara nyingi twajihesabu wenye haki,huku tukijificha chini ya mwongozo wa "kushikilia bendera ya Ukweli" au "kwa kutetea Ukweli."
===================
R5284
MAFUNDISHO YENYE UMUHIMU ZAIDI AU YASIO NA UMUHIMU ZAIDI
Kuna vipengele fulani ya mafundisho ya Kristo ambayo ni ya msingi na ya lazima, na bila hayo, mtu hawezitambuliwa na Bwana kama mmoja wa wafuasi wake. Kuna huduma zingine ambazo zinaweza kuonekana kuwa nzuri,ya msaada, ya baraka, lakini sio ya msingi - sio muhimu kwa ushirika katika Mwili wa Kristo. Lakini mafundisho yalio ya msingi yamefurahiwa na watakatifu walio wema ,tangu Siku ya Pentekosti hadi sasa.
Sisi, ambao ni sawia na darasa lile kwa wakati huu, tuko chini ya mafundisho hayo hayo ya msingi, na tumepewa kibali, neno la ukweli, "chakula kwa wakati unaofaa," kwa uimarishaji wetu. Hizi mwisho sio muhimu kwa ushirika wetu katika Mwili wa Kristo; la sivyo babu zetu ambao hawakuwa nao wasingekuwa washirika wa Kristo,na kungekuwa hakuna Mwili wa Kristo kwa karne nyingi.
Nadharia ya msingi ya Upatanisho ni kama ifuatavyo:
(1) Wanadamu wote - watoto wa Adamu - ni wenye dhambi.
(2) Hakuna anayeweza kupatanishwa na Mungu bila dhabihu ya Mkombozi.
(3) Yesu alikuja ulimwenguni kuwa Sadaka - na baadaye kutumia bei ya Fidia kwa dhambi za ulimwengu.
(4) Kwa msingi wa imani katika kazi ya Mkombozi, mwamini anaweza kujitolea kwa huduma ya Kiungu, kwa kukubali mwaliko wa Kiungu, "Toa miili yako iwe sadaka hai."
(5) Kwa kufanya hivyo, mwamini anaweza - hadi wakati wa kukamilika kwa Nambari ya wateule - tekeleza dhamana kamili ya imani kwamba dhabihu yake itakubaliwa na Baba; na kwamba atapokea mgao wa upako wa Roho Mtakatifu -yaani kuzaliwa.
(6) Wale ambao wamekidhi masharti haya wanapaswa kukubaliwa kama ndugu kwa nama ya hali ya juu. Hii inaweza kuonekana kuwa muhimu kila wakati, na zaidi ya hii tunaamini sio lazima leo. Lakini ikiwa kwa sababu ya siku zetu nzuri tuna maarifa zaidi, tunaweza pia kuwa na majaribio yanayolingana nayo, ambayo maarifa yetu makubwa yatasababisha.
Ushauri wetu kwa watu wapendwa wa Bwana kila mahali ni kwamba wasiweke nira juu ya kila mmoja, zaidi ya misingi iliyoainishwa hapo juu - kwamba vinginevyo wakasimame huru, na wakawachane huru, na wakishirikiana na kukubaliana kadri wanavyoweza.
Ikiwa kuna nia ya kusongana kila mmoja juu ya imani hii ya kimsingi, na ikizingatiwa kuwa ni muhimu kujitenga ili kuafikia maendeleo ya pande zote, basi bila shaka badala ya ugomvi wa kawaida kujitenga itakuwa njia ya busara.
[…]
Ikiwa baada ya kuzingatia mambo haya kikamilifu, darasa litagundua kuwa haliwezi kukubaliana, na ingefanya maendeleo bora kama madarasa mawili, tungekubaliana katika hitimisho hilo kama la busara, kadiri tunavyoweza kuona umuhimu wa mgawanyiko. Mgawanyiko kama huo hautahitaji kutenganisha kikundi chochote kutoka kwa watu wa Bwana, au kutoka kwa Jamii, kwa sababu wote wanamkubali Yesu kama Mkombozi wao, na wote wawili wanakubali kwamba damu yake ina nguvu kabisa.
====================
Unaweza kuwa unafikiria "Je! Unaenda wapi na hii?"
Ndugu, tuko kwenye njia panda. Tumedanganywa kwa kufikiria kuwa vitu kama Chronolojia, au Mchungaji, au Ufalme ndio vinatufanya kuwa tofauti - hata bora kuliko "wakristo wa kawaida" hao wanaoogopwa.
Huo ni uwongo, uliojengwa tukwenye miali ya kiburi, iliyochochewa na baba wa uwongo. Ni UWONGO ambao inatupa hisia za uwongo za kisalama. Ni uwongo ambao umewasumbua marafiki wetu wapenzi katika Mashahidi wa Yehova kwa mda mrefu ya karne hii. SIO wingi wa kile tunapenda kuiita "chakula kwa wakati wake" ambayo inafanya sisi tofauti.
Sio. Hata. Karibu yake.
Kwa hivyo, ni NINI hutufanya kuwa tofauti - au labda ikiwekwa kwa usahihi zaidi, ni nini kinapaswa kutufanya tofauti?
Kuna sehemu MOJA tu ya kugeuza - katika Neno Takatifu la MUNGU.
Psa 51:10 Ee Mungu, uniumbie moyo safi;
Uifanye upya roho iliyotulia ndani yangu.
Luk 18: 10-14 KJV
10 Watu wawili walikwenda Hekaluni kusali; mmoja alikuwa Mfarisayo, na mwingine ni mtoza ushuru.
11 Yule Mfarisayo alisimama na kuomba hivi na yeye, Mungu, nakushukuru kwa kuwa mimi si kama watu wengine, wanyang'anyi, wasio waadilifu, wazinzi, au hata kama huyu mtoza ushuru.
12 Mimi nafunga mara mbili kwa juma, ninatoa zaka ya yote ninayo.
13 Lakini yule mtoza ushuru alisimama mbali,wala hakuthubutu hata kuinua macho yake mbinguni, lakini akapiga kifua chake, akisema, Mungu unirehemu mimi mwenye dhambi.
14 Nawaambia, mtu huyu alishuka kwenda nyumbani kwake akiwa amehesabiwa haki kuliko yule, kwa maana kila ajikwezaye atadhiliwa, naye ajidhiliye atakwezwa.
Uwe MTOZA USHURU !!! Sio Mfarisayo…
Vipi? Je! Tunamfutaje Farisayo kutoka kwetu? Kwa kushukuru, hatuitaji kuangalia mbali, na sio lazima tujue mengi!
Imeonyeshwa mara nyingi hapo awali kuwa kile tunachokiita "Mafundisho ya Yesu mlimani" inaweza pia kuitwa "mitazamo tunayopaswa kuwa" au "Tabia ya".
Hizi ni mambo Yote ya moyo, SIYO YA KICHWA/MAWAZO! Haleluya kwa hiyo!
Mat 5: 1 Alipoona makutano, alipanda mlimani. Alipokuwa ameketi, wanafunzi wake walimwendea.
Fikiria kwa makini, Yesu anazungumza na nani? Sio "umati wa watu," bali wanafunzi wake wa karibu. Kwa kweli, alikimbia umati wa watu na iliwabidi wanafunzi kumfuata mlimani.
Mafundisho ya Yesu Mlimani
Mat 5: 2-3
2 Akafunua kinywa chake, akawafundisha, akisema,
3 Heri walio maskini wa roho; maana Ufalme wa mbinguni ni wao.
Neno la Kiyunani lililotumiwa mwanzoni mwa kila Fundisho lilikusudiwa kufikisha wazo la baraka ULIOKITHIRI. Hili sio tu wazo rahisi la kubarikiwa au kuhisi kubarikiwa. Hii ni kwa maana ya juu zaidi - ambayo ni kwa maana kamili na ya mwisho, baraka hiyo itakuwa thawabu ya kuwa sehemu ya Bibi-arusi, Uungu wa Kiungu.
Neno la Kiyunani la "masikini" pia liko kwenye maana ya JUU ZAIDI. Inamaanisha kabisa umaskini. Beggarly, pauper - hii inaashiria unyenyekevu wa KIHAKIKA!
Mat 5: 4 Heri wenye huzuni, kwa maana watafarijiwa.
Neno la Kiyunani la "kuomboleza" hapa linaonyesha hali ya kuomboleza sana, sio huzuni ya kawaida au huzuni ya mara kwa mara. Hii ni hali ya kudumu, ya kuvunjika moyo kwa ajili ya dhambi zetu WENYEWE, hali mbaya. Jinsi tunavyoendelea, utaanza kugundua mfumo unao ujengeka, kwamba kila moja ya haya mafundisho sio mambo yanayojipanga kivyao pasina kuhusisha yale mengine , lakini badala yake ni ya jumla, na kwamba kila mmoja yao itapatikana katika KILA ujumbe wa ile kundi ndogo.
Mat 5: 5 Heri wenye upole, Maana hao watairithi dunia.
Usifanye makosa ya kudhani kwamba upole huu ni udhaifu. Wengi wa watu walio na upole pia ni watu wenye uhodari SANA. Musa, “mtu mpole zaidi katika ulimwengu wote” na Yesu “mpole na wanyenyekevu” hawakuwa waoga. Mtu mpole sio mtu rahisi anayesukumwa sukumwa kwa urahisi. Upole unaturejesha kuwa “masikini wa roho.” Ni utiifu kamili, pasina upingamizi wowote, kwa Mapenzi ya Mungu. Upole huongoza mawazo na hisia ya mtu k.v. - upole, kujidhibiti, kutokukasirika, uvumilivu katika kuumia au kukasirika - wakati huo wote akitumia mafunzo hayo kwa kujenga tabia yake mwenyewe.
Mat 5: 6 Heri wenye njaa na kiu ya haki, maana watashibishwa.
Maelezo moja ya maoni: HII ya njaa ni ya haki KIKAMILIFU, sio ya kiasi tu ya kutuliza dhamiri iliyo na hatia.
Neno la Kiyunani la "njaa" hapa sio lile tunalofikiria kama njaa. Ni njaa isiyoweza kukomeshwa, isiyoelezeka, isiyoweza kujazika ambayo haiwezi kutosha. Je! Si ni jambo la kushangaza kwamba hatuli vitu ambavyo hatupendi? Ikiwa tunapenda ladha ya dhambi, au raha, au ya pesa, au ya uovu – hebu fikiria ni nini tutakula?
Nilikuwa nikifikiria na kusema vitu vya kijinga kama: Ni rahisi kupenda haki, lakini ni kuchukia uovu ndiyo nang’ang’ana nayo.
Ndio ... Sina ueledi sana. Huo ni adui anayepanda mawazo hayo mabaya kichwani mwangu, kama njia ya kunifanya nihisi vizuri juu yangu mwenyewe.
Ukweli ulio wa NDANI pia mara nyingi huwa chungu sana kukutana nao. Hakika sisemi juu ya unabii au nyakati, lakini haswa ukweli juu yetu sisi na jinsi ukweli huo inavyotushawishi katika ndani ya mioyo yetu.
Kwa kifupi, HUWEZI "kupenda haki" PASINA" kuchukia uovu!" Haiwezekani. Kuchukia uovu kwetu ni SAWASAWA ikilinganishwa na UPENDO wetu kwa haki.
Mat 5: 7 Heri walio na rehema, kwa maana watapata rehema.
Hapa aya nyingine ya "sawia". Kwa maneno rahisi, "unapata kile unachotoa." Huu sio rehema ya kulazimishwa, au rehema ya mazingaombwe. Hatuwi na huruma ndio tutarajie malipo, lakini huruma huo unakuwa kama jiwe la thamani katika safu hii ya vito ambavyo tunapaswa kujitahidi kufunga shingoni mwetu.
Ni karibu ya hisabati kwa asili na usahihi wake, na pia inatupa picha ya tabia ya ajabu ya MUNGU wetu – Abba baba yetu . Yeye hutupa nguvu na funguo za ufalme, kichocheo cha siri au fomula ya kufanikiwa – kwa kadri tunavyoonyesha rehema, vivyo hivyo tunaonyeshwa rehema. Kadiri tunavyowasamehe wale ambao wametukosea, vile vile tunasamehewa zaidi tunapokosea MUNGU. Pia, huwezi kuwa mwenye huruma au kusamehe bila kuwa na unyenyekevu, upole, na kuwa maskini kiroho - yote haya yanajumuishwa kwa kiwango kubwa lile neno la herufi nne kwa lugha ya Kiingereza:
L-O-V-E- yaani UPENDO.
Kuwa maskini katika roho, kuwa na huzuni, tabia ya kuhuzunisha, kuwa mpole, njaa ya haki, na kuwa na huruma kunatuweka kwenye mwendo wa mgongano na Tabia inayofuata ya…
Mat 5: 8 Heri wenye mioyo safi, Maana hao watamwona Mungu.
Je! Umewahi kufikiria juu ya wakati UNAMWONA MUNGU mara ya kwanza kabisa?! Kwa macho yako mwenyewe, sio ya kimantiki au ya mfano, lakini unamuona jinsi alivyo? Kwa hakika mimi nina dhana hiyo! Ama Je! Wewe una kitu unachotaka zaidi?
Yesu anatuweka - Wanafunzi wake - Kichocheo cha Siri cha Mtu Mzuri wa Tabia. Mafundisho haya ya Yesu yakizingatiwa yanaweza kusaidia kusafisha mioyo yetu. Yanaweza KUSAIDIA kupata matokeo hayo! Hebu fikiria, ingekuwaje kuwa na moyo SAFI kabisa! Ni ngumu kidogo kupata ile picha kamili.
Lakini tena izingatiwe kwamba, hii ni kwa KANISA, ambao watamwona MUNGU kwa macho yao!
Pendaneni KWA BIDII moja kwa mwengine kwa moyo ulio SAFI!
Mat 5: 9 Heri wapatanishi; Maana wataitwa wana wa Mungu.
Aya hii haizungumzi juu ya kuishi KWA amani,lakini ni juu ya wale ambao wanaendelea kuchukua hatua ili kushinda uovu, ugomvi, nk ili KULWETA amani. Hili laweza kuwa katika nyumba zetu wenyewe, katika eklesia zetu, mahali pa kazi, nk Kwa kufanya hivyo, pia tunaleta amani na MUNGU. Mpatanishi hawi chanzo cha mng’ang’ano, ugomvi, mazungumzo maovu na hashiriki au kuhimiza mambo kama hayo - ila kwa wakati kanuni ya kweli, sio kanuni ya kujipalia, iko hatarini. Mpatanishi hua tayari kila wakati kutoa hiari za kibinafsi, uhuru, na hata "haki" kama dhabihu juu ya madhabahu ya upendo kuleta amani, bila kunung'unika. Kwa kufanya hivi, tuna hakika kwamba sisi ni "watoto wa MUNGU" kweli.
Mat 5:10 Heri wenye kuteswa kwa ajili ya haki; Maana Ufalme wa mbinguni ni wao.
1Tim 3:12 - WOTE wanaoishi kiungu katika Kristo Yesu watateswa. Iwapo tutajikuta tukikubaliwa na ulimwengu na kuishi kwa maelewano kamilifu katika maisha yetu ya kila siku pamoja na watu na wandugu, basi tunaweza kuwa katika shida zaidi kuliko tunavyojua. Iwapo hatuonekani kuwa wa kipekee au wasio wiyiana kwa njia fulani na wale wanaotuzunguka - ikiwezekana hata kati ya ndugu zetu wenyewe - basi hii inaweza kuonyesha kuwa kweli tuko katika hali mbaya. Kumnukuu Mchungaji: "Sio tu kwa mateso mazito, lakini hata kwa yale madogo, wakati majina yetu yanaonekana kama mabaya" wakati watu watawatenga na shirika zao. "
Ulimwengu utapenda walio wake. Ikiwa ulimwengu unatupenda, basi sisi sio wa Mungu.
Mat 5:11 Heri ninyi, watu watakapowashutumu na kuwatesa, na kuwanenea kila neno baya kwa uongo, kwa ajili yangu.
IKIWA Injili - Habari njema - ndio mada yetu KUU maishani, basi italeta kukataliwa na mateso. Mungu wa ulimwengu huu anachukia Injili. Injili haiendi sambamba na yote ambayo yeye na ulimwengu huu husimamia. Haipaswi kuwapo na utata wowote baina yetu na wale wanaotuzunguka kuhusu msimamo wetu. Giza LINACHUKIA nuru.
Basi wacha wote tuwe wana wa nuru!
Mat 5:12 Furahini, na kushangilia; kwa kuwa thawabu yenu ni kubwa mbinguni; kwa maana ndivyo walivyowatesa manabii waliokuwako kabla yenu.
Thawabu yenu ni kubwa mbinguni! Hakuwezi kuwa na swali au mjadala juu ya ni kwa nani "Mafundisho haya" yamelengwa. Kama tulivyosema hapo awali, haya YOTE ni
mahitaji ya ukuzaji wa tabia na YOTE yatapatikana kwa wingi katika Kila. Moja. Yao. Katika lile kundi ndogo.
Chumvi na Nuru
Mat 5: 13-16
13 Ninyi ni chumvi ya dunia; lakini chumvi ikiwa imepoteza ladha yake, itatiwa nini hata ikolee? Haifai tena kabisa, ila kutupwa nje na kukanyagwa na watu.
14 Ninyi ni nuru ya ulimwengu. Mji uliojengwa juu ya mlima hauwezi kusitirika.
15 Wala watu hawashii taa, na kuiweka chini ya pishi, bali juu ya kiango; nayo yawaangaza wote waliomo nyumbani.
16 Vivyo hivyo nuru yenu na iangaze mbele ya watu, wapate kuyaona matendo yenu mema, wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni.