SURA YA KWANZA--Chapter 1
SURA YA KWANZA
HALI YA UKRISTO WA KISASA
Ukristo wa Kidersturi, Je! Biblia Inasema Nini, Shida ya Ujinga
Kabla ya kuangalia shida maalum zinazoletwa na kile nitakaoita Ukristo wa kidersturi kuanzia hapa kwendalea. Kwanza nataka kushughulikia shida ya mtazamo mbaya ambao wengi huwa nao kuhusu imani. Wengine wanafikiria kuwa ukiwa “mtu mzuri” (asiekubali maovu), imani yako inatosha. Ukweli ni kwamba, unaweza kuwa hata si Mkristo kabisa lakini unamaadili mema. Mtu anaweza shikilia imani ambao tamaduni imetawala pasi na kuelewa. Vile vile unawezakuwa unafahamu sana kanuni za kimsingi za Kikristo lakini usiweze kufahamu jinsi kanuni hizo zinapaswa kutumika katika maisha yako.
Natumai hufikirii kuwa ninajivuna, au kuwa mkali sana kwa wale Wakristo wa kidersturi. Hebu tazama ukweli, Je! Hao Wakristo wa kidersturi huwa wanaona kweli umuhimu wa imani ya Kikristo? Na Je! Huwa wanaitumia kama kigezo wanapokufundisha watoto wao maadili? Si huwa wanasisitiza kwamba watoto wao wapate elimu nzuri tu, kuliko kujifunza juu ya mambo ya Mungu? Si huwa wanaona aibu tu iwapo watoto wao wamekosa elimu nzuri?
Basin na kama watoto wao wana uelevu wowote wa imani ya Kikristo, labda wameipata wenyewe; na iwapo watoto wao wanajiona Wakristo, labda sio kwa sababu wamejifunza ukweli na kufikia hatua ya kushawishika, ila ni kwa sababu familia yao ni ya Kikristo, kwa hivyo wanaamini ni lazima na wao wawe Wakristo.
Sasa shida na dhana kama hii ni kwamba, imani halisi haiwezi kurithiwa. Ukristo ukizingatiwa kwa njia hii, kwa mfano, inaweza fanya vijana chipukizi, bila shaka, kuaacha imani hii "iliyorithiwa”, na ambayo katu hawawezi kuitetea. Iwapo watafikishwa hatua ya kuhojiwa ukweli wa Ukristo wao au wakutane na pingamizi, kwa mfano wanaweza ingia katika mjadala na wenzao waumini na katika ushirika huo, wajipate hawawezi kujibu kwa busara hoja za Kikristo ambazo wapinzani wao wanawakabili nazo. Laiti wangefahamu ukweli wanaoiamini na kwa ni nini wanaiamini, mambo kama haya hayangetikisa imani yao hata kidogo.
Nahofia hatima ya imani halisi katika kaunti yetu. Tunaishi katika nyakati ambazo mtu wa kawaida hapa nchini kwetu anashawishiwa kirahisi na namna wasomi wanavyoueneza ujumbe wa kupinga Ukristo. Yatupasa kutazama yaliyotokea huko Ufaransa na kujifunza kutokana nayo.1 Katika nchi hiyo, kundi fulani liliwashambulia Wakristo sana na kuwapotosha, kwa sababu hao Wakristo waliodai imani hawangeweza tetea imani hio kutokana na shambulio hio, hata ijapo hoja za washambuliaji hao zilikuwa na kasoro nyingi. Tunafaa kushtuka kwamba mafundisho katika imani halisi yamepuuzwa, ikiwa hayajafutwa kabisa, kutuka shule zetu na vyuo vikuu.
Kama ni hivyo, si inashangaza kwamba hali ya kiroho ya nchi yetu ina umuhimu mdogo sana hasa kwa wale ambao hata hawaelimishi watoto wao juu ya Ukristo wa kweli? Tabia zao zinaonyesha kutokujali kwao; sio tu kwa hali ya Ukristo katika nchi yetu tu, bali pia hata na haja ya kupeleka ujumbe huo wa Kristo katika sehemu zingine za ulimwengu ambako hawana ukweli huo.
Wengine wanaweza kusema kwamba imani ya mtu ni jambo la kibinafsi na haipaswi kuzungumziwa hadharani. Wanaweza sinikiza msimamo huo kwa watu ndio, lakini, ni madhumuni gani hasa wanao mioyoni mwao? Ukweli ni kwamba, wale ambao wanasema hayo, kwa kawaida hawazingatii kabisa mambo ya imani maishani mwao, na ukichunguza mioyo yao habari za imani halisi hazipo kabisa. Mungu hayupo popote katika matumaini, hofu, furaha au huzuni yao, au katika mafanikio, utajiri na mali yao; ila hawaoni uwezekano kwamba haya yote ni ishara za upaji wa Mola. Na iwapo wanampa Mungu sifa, kwa kawaida waifanya kwa njia inayoonyesha kuwa maneno yao hayana uzito wowote.
Mazungumzo yao yanapochemka, utaona ni jinsi gani Ukristo wao hauhusiani kabisa na imani iliyofundishwa naye Bwana wetus Yesu. Kila kitu kinajitenga na kusimama peke yake. Tabia zao hazipunguki dhidi ya vigezo vilivyowekwa na injili. Wanaendeleza falsafa yao wenyewe, ambao wanajaribu kuifanya kama imani ya Kikristo.
Shida kubwa na kesi aina hizi ni kwamba hawa watu wana desturi ya kuafikia hitimisho pasi na kuchunguza maandiko. Bibilia inakaa vumbi kwenye rafu zao. Watu hawa hawajui kusoma na kuandika. Ujuzi wao wa Bibilia ni ule wa watoto wachanga.
Tungekuwa tofauti iwapo mfumo wetu wa maadili ungekua na msingi wa Kibibilia badala ya vigezo vilivyowekwa na Wakristo wa kidersturi. Ingekuwa jambo la kupendeza kuona mwitikio wa wake kwa waume ambao wamelainisha tabia zao sambamba na vigezo alivyoweka Mungu. Waandishi wengineo wa wakati wetu pia wamejaribu kuangazia jambo hili. Ijapo wameelezea ukosefu wa imani kubwa ya kidini, mara nyingi wamekuwa wakishughulikia suala hilo kama mojawapo ya habari isiyo na umuhimu wowote pasi na kushughulikia suala kubwa zaidi la hatari hii inayoletwa na imani hiyo duni. Haya ni maswala yanayohusu umilele. Hayafai kuchezea.
Inakubidi kujihoji kwamba Mungu anafikiri nini kuhusu haya yote. Hapo awali nilifanya uchunguzi na nikapata kwamba siku moja tutalazimika kutoa hesabu ya vile tulivyoishi na pia vile tulivyotumia vipawa alivyotupa Mungu. Kwa kuwa Mungu anayazingatia sana mambo haya, hakika tutawajibika Kwake kwa vile tulivyotumia nafasi nzuri ya kujifunza ukweli wa imani halisi na mafundisho yote kuhusu ukweli huo tuliopokea. Lazima nishangae na kujiuliza Mungu anafikiri nini kuhusu ujinga wetu wa hiari kwa mambo haya.
Kuelewa Ukristo sio kitu ambacho huja bila juhudi. Karibu kila mfano katika ulimwengu wa asili inatufundisha kanuni hii. Basi jinsi tunavyojitahidi kufurahia vitu vyote vizuri ambavyo Mungu ametupa, na vivyo pia yatupasa kutia bidii ili tupate kuelewa ukristo wa kweli. Hakuna anayewezakutarajia mafanikio kielimu, kisanaa, kifedha au katika riadha pasi na bidii na pia uvumilivu.
Huwa tunatumia maneno haya mara nyingi "Lazima uitake! '' Lakini cha mno ni kwamba ukomavu wetu katika imani kunahitaji kanuni hio hio. Msingi wa Ukristo ni ufunuo kutoka kwa Mungu ambao umejaa habari ambayo mtu wa kawaida hawezi kufikia. Utajiri wa maarifa haya hauwezi kuwa bora bila bidii.
Kujifunza Bibilia kwa uangalifu kutatufunulia ujinga wetu wenyewe kwa mambo haya. Changamoto kuu tunao ni kukataa uelevu wa Ukristo wa juu juu, na kusisitiza kwamba sio muhimu kuwa mtu wa kidini tu au kuwa mtu wa maadili mema tu, bali muhimu zaidi ni kuelewa vizuri elimu ya kibiblia, kuelewa namna ya kuunganisha kanuni hizo katika maisha yetu kimaadili, na pia kuelewa namna ya kuweka katika matendo kile ambacho tumejifunza.
Bibilia ni mojawapo ya vipaji kuu vya Mungu kwa wanadamu na inatueleza juu ya KIPAJI kilicho kubwa zaidi ya yote ambacho wanadamu wamekuwa wakimtamani katika enzi zote na ambacho manabii walikizungumzia karne nyingi zilizopita –yaani Mwokozi wetu Yesu Kristo. Wakati Yesu hatimaye alikuja, kuwasili kwake kulisifiwa na malaika kwa shangwe wakisema, "Utukufu kwa Mungu aliye juu zaidi, na amani duniani kwa watu wote ambao kwao kibali chake kinakaa" (Luka 2: 14). Unawezaje kupima thamani ya habari hii njema ya Kristo? Katika Bibilia habari hio imetajwa kama nuru gizani, uhuru wa kutoka utumwani na uzima kutoka mautini. Angalia jinsi kanisa la kwanza liliuthamini ujumbe huo. Waliupokea kwa shangwe na shukrani kubwa.
Ama kweli mambo haya yote yanapasa kutusaidia kuona thamani isiyo na kifani ya imani ya kweli. Karama kuu ya Mungu mara nyingi hukataliwa kabisa au kutendewa kana kwamba haifai. Lakini iwapo kweli tungeanza kuchunguza Biblia, tungestajabia thamani halisi ya karama hii. Pengine inaonekana kuwa ni jambo la kawaida kwetu kuwahimiza watu kujifunza Biblia. Lakini Bibilia yenyewe inazungumza maneno magumu kwetu kama, " Mwetayari siku zote kumjibu kila mtu awaulizaye habari za tumaini lililo ndani yenu;" (1 Pet.3: 15). Waliokwisha kufanya hivyo wanatueleza kuhusu thamani iliokuu inayotokana na juhudi kama hizo. Bali sio hao wengi walio na Bibilia kwenye rafu majumbani mwao, kwa maana yaliyomo ndani ya Kitabu hicho bado ni siri kwao. Matokeo yake ni kwamba katika ulimwengu wa Ukristo hapa Magharibi, tumeshikilia namna ya Ukristo wa kidesturi ambao ni mbali kabisa na swala halisi.
Sineni juu ya wasioamini hapa. Ninazungumza juu ya wale wanaosema kuwa wanaamini Bibilia ni Neno la Mungu na ambao wanadai wamekwisha mpa Yesu Kristo maisha yao. Lakini wako katika imani ya kawaida. Wanakubaliana na kanuni potovu kama, "Haijalishi unachokiamini, kilicho muhimu ni jinsi unavyoishi " na " Unayoamini si hoja, maadamu u mwaminifu katika imani yako." Huu ni ujinga ulioje!
Kile tunachoamini huamua jinsi tunavyoishi. Wanaoshikilia kwa dhati msimamo kwamba wanachokifanya ni sahihi mara nyingi ndio husababisha maafa makubwa zaidi ya jinai dhidi ya wanadamu. Tena tukio la hivi majuzi huko Ufaransa hutumika kama mfano wazi wa ukweli huu. Karibu watu wote wanaamini wanaishi maisha mema na yenye maadili. Ila wanapima maisha yao dhidi ya vigezo kadhaa vya kujifanya bila kugundua kuwa mara nyingi maovu ni bidhaa ya ujinga au makosa. Watu kama hao mara nyingi wanakosa uwezo wa kutofautisha mema kwa mabaya au ukweli kwa makosa.
Hii ndio sababu mojawapo ya umuhimu wa kujifunza Bibilia kwa bidii. Hapo ndipo Mungu ametupa maagizo hitajika kutuwezesha kupambanua mema na mabaya au ukweli na makosa. Pasi na kuelewa kanuni na maagizo yake, tunakuwa wahasiriwa wa ujuaji wetu. Je! Faida ya ujanja ni nini ikiwa dhamiri yetu imewashwa, mioyo yetu imeumizwa, na akili zetu zimepofushwa kiasi cha kutoweza kupambanua maadili?
Imani ya kweli inahitaji akili timamu, utumiaji thabiti wa njia ya maarifa na mafundisho, unyenyekevu unaosababisha hamu ya kufundishwa, na hitimisho lisilo na ubaguzi juu ya kile uchunguzi huu unaonyesha. Ikiwa tutatumia mbinu hii kusoma Biblia, basi Mungu atatimiza ahadi zake. Pia iwapo tutatafuta na kuendelea kutafuta, basi tutapata; na iwapo tutauliza na tunaendelea kuuliza, tutapokea; pia tukigonga na kuendelea kugonga, mlango wa ukweli utafunguliwa. Je! Tunawezaje kukataa ofa kama hii?
Ila fursa kama hiyo huambatana na jukumu. Lakini tukichagua Ukristo wa kidesturi tu, na kubaki wajinga wasiojali imani halisi, basi ni vipi tutaweza kumshawishi Mungu?
Kumbuka
1. Wilberforce hutumia Ufaransa kama mfano wa jamii ya wagonjwa. Mnamo 1797, wakati kitabu hiki kiliandikwa hapo awali, Uingereza ilikuwa bado inapigana na vikosi vya mapinduzi vya Ufaransa ambavyo vilikuwa vinajaribu kushinda Ulaya. Mapinduzi ya Ufaransa yalikuwa yameathiri sana utamaduni na maadili ya Ufaransa. Wilberforce hutumia hii kama kielelezo cha kile kinachoweza kutokea Uingereza.