SURA YA PILI
MAWAZO YA KISASA KUHUSU ASILI YA MWANADAMU
Sehemu ya Kwanza: Dhana Potovu Kuhusu Hali Halisi ya Kibinadamu
Baada ya kutazama ukosefu wa uelevu uliopo kati ya Wakristo wa kidesturi kuhusu umuhimu wa imani halisi, kwa sasa tuangalie maoni hasi walionao Wakristo wengi kuhusu hali halisi ya kiroho ya kibinadamu. Hili ni swala ambalo wengi wanaosoma kitabu hiki wanaweza kuwa hawajatilia maanani sana. Ikiwa hiyo ndio hali kwako, basi, nakuuliza uzingatie kwa makini yale yanayofuata. Maana hii ni mada muhimu sana. Ukweli wa somo hili uko ndani ya imani yote ya kweli.
Ni maoni yangu kwamba wengi wa Wakristo hupuuza, au wanakanusha au, angalau, hupunguza utata kuhusu ni nini maana ya kuwa mwanadamu aliyeanguka. Wanaweza kukubali kuwa ulimwengu daima umejawa na uovu na mauovu na kwamba tabia za watu daima huelekea kwa tamaa na ubinafsi. Wanaweza pia kukubali kwamba matokeo ya ukweli huu ni kwamba katika kila kizazi tunaweza pata visa vingi vya ukandamizaji, ukatili, ukosefu wa uaminifu, wivu na vurugu. Vile vile wanaweza kukubali kuwa huwa tunatenda hivi hata tukiwa timamu.
Mambo haya ni kweli; hatuyakatai. Yako wazi kiasi cha kutatanisha ni kwa nini wengi bado wanaamini kwamba kuna wema katika asili ya mwanadamu. Lakini ingawa ukweli unaweza kukubaliwa, chanzo cha ukweli huo bado kinaweza kukataliwa.
Vitu hivi vinaweza zingatiwa kama shida ndogo ndogo au shida za mara kwa mara. Hayo maelezo mengine yanayotolewa hayaelezei uhakika wa mambo haya. Kiburi cha mwanadamu siku zote humkataza kuukabili ukweli. Hata wengi wa wale wanaodai kuwa ni Wakristo huwa wanafikiri kwamba mwanadamu kwa asili yake huwa mwema ila ni nguvu za majaribu tu humsukuma mbali na njia. Wanaamini kuwa dhambi na uovu ni maswala tofauti kabisa, na wala hayahusiki na sheria.
Lakini Biblia inatuonyesha picha tofauti kabisa. Lugha ya maandiko matakatifu sio kwa watu wanaozimia moyoni. Maandiko yanatufundisha kwamba mwanadamu ni kiumbe aliyeasi, aliyeanguka kutoka kwa asili yake ya mwanzoni, aliyepotoka katika asili yake, mwovu wa fikira, aliyeegemea uovuni na wala sio katika wema, na aliyeathirika na dhambi hata mpaka kwenye msingi wa uhai wake. Ukweli kwamba hatutaki kukiri ukweli huu ni dhibitisho ya hali hio yao. Kama vile Milton alivyosema katika kitabu chake Paradise Lost.
Je! Unaona ni kwa kina gani?
Anguko hilo ni wa kutoka urefu gani1
Hebu tafakari juu ya uwezo wa ajabu wa akili ya mwanadamu. Tuna nguvu ya kubuni, kuuliza, kufanya uamuzi, kukumbuka yaliyopita, kufanya uamuzi kwa sasa na kufanya mpango wa siku zijazo. Kwa kutumia uwezo wa kufumbua mambo, hatuelewi kitu tu; bali pia tunaweza kukisifia, haswa ikiwa ni kitu kizuri chenye ubora wa maadili. Katika hisia, tunaouwezo wa kuogopa na kutumaini, uzoefu wa kufurahi na kuhuzunika, pia huruma na upendo. Na tukitaka, pia tunaweza kufanya kazi ngumu bila uoga wowote huku tukijitahidi kwa bidii. Kwa nguvu ya dhamiri yetu, tunaweza chunguza mawazo na hamu ya mioyo yetu na kutumia akili zetu kudhibiti tamaa zetu. Ama kweli sisi tu viumbe vya ajabu. Iwapo wageni toka ulimwengu mwingine wangetutazama, watastaajabia uwezo wetu wa kutumia fahamu hizi zote kuwa bora zaidi ya vile tunavyoweza kuwa. Wangefikiria kwamba muumbaji wetu angefurahi kwa mema yote ambayo tungechagua kufanya na sifa hizi za ajabu.
Kwa bahati mbaya, sote tunajua kuwa mambo hayawi hivyo. Hebu tazama jinsi tunavyotumia nguvu hizi. Rejelea tu hapo awali kidogo ukatazame taswira kuu ya historia ya wanadamu. Je! tunaona nini? Tunachoona ni kwamba kusudi maalum la mwanadamu limebatilishwa. Tamanio la wanadamu limepotoshwa. Hasira, wivu, chuki na kulipiza kisasi huinua vichwa vyao mbovu. Tumekuwa watumwa wa asili zetu za chini na inaonekana kuwa hatuwezi kufanya vyema!
Historia inathibitisha misiba hii ya asili ya wanadamu. Ustaarabu wa jadi haukuwa na sifa nzuri. Kinyume chake, hata tamaduni zilizoendelea zaidi zilifunikwa kwa giza la maadili. Tunapata ushirikina, ukosefu wa hisia za asili, ukatili wa kupindukia, ukandamizaji usio na huruma na ukatili mkubwa kila mahali tunapotazama. Hatuoni adabu na maadili zikitawala popote. Kwa maneno ya Paulo, “Basi Mungu aliwaacha katika tamaa za mioyo yao, waufuate uchafu, hata wakavunjiana heshima miili yao '' (Rom1:24).
Na hata tukigeuza macho yetu tuanze kutazama hali ya kisasa, tunapata hali ni hiyo hiyo. Mwanahistoria mmoja akaelezea juu ya Marekani kwa njia ifuatayo:
Ni uwanja wa kiburi, na uzembe, na ubinafsi, na ujanja na ukatili; kamili ya kisasi ambacho hakuna kitu kinachoweza kukomesha, kwa ukali ambao hakuna kitu kinachoweza kutuliza; hisia nzuri zaidi ya asili ni geni kwao. Wanaonekana hawawezi kupendana upendo wa ndoa, au kupenda wazazi, au heshima za kifamilia, au uhusiano nzuri wa kijamii; ikijumuishwa pia na hali yao ya upotovu, pamoja na tabia mbovu nyingi za udhaifu wa jamii iliyochafuliwa. Namna wanavyowadhulumu mateka waliochukuliwa vitani, wanavyokusanya miili yao na kuisherekea, baada ya kuwatesa vibaya sana na kuwauwa; yote hayo yanajulikana wazi, na haina haja kurudia simulizi hiyo ya tabia hio mbovu ya chukizo. Na wala hakuna sifa zozote za kupendeza zinazoweza kufuta picha hii mbaya, isipokuwa uhodari, na uvumilivu, na bidii kwa ustawi wa jamii yao ndogo, ikiwa wema huo wa mwisho, uliotekelezwa na kuelekezwa kama ilivyofaa, unaweza kufikiriwa kuwa unastahili kupongezwa.2
Hata katika mataifa yenye ustaarabu zaidi tunaona ukweli wa asili ya wanadamu walioanguka. Katika baadhi ya mataifa haya, ushawishi wa Kikristo umeweka viwango juu zaidi kuliko ile tunayoelewa kuwa ni mataifa kafiri. Kwa jumla, ushawishi wa Kikristo katika mataifa umeboresha tabia na starehe za jamii, haswa kuhusu maskini na wanyonge, ambao wamekuwa wakipewa umakinifu wa pekee na wale wanaodai imani ya Kikristo. Ushawishi huu umesababisha baraka nyingi kwa watu wengi ingawa watu hao wanakataa ukweli wa Biblia na hawakubali mamlaka yake. Lakini hata katika mataifa hayo ambayo yameshawishiwa na imani ya Biblia, tunaona mifano mingi ya udhalimu wa kibinadamu.
Asili kamili ya mwanadamu inapofichuliwa katika hali ambapo ushawishi wa Kikristo ulikwisha shamiri, udhalimu huwa dhahiri zaidi. Sheria na dhamiri ya jamii kama hizo huundwa ili kudhibiti nguvu hizi za asili ya uwanadamu. Sheria hizi zikiondolewa au kukiukwa, tunaona uhalifu mbaya zaidi ukitekelezwa mchana peupe hata bila aibu.
Unapozingatia mafundisho ya kiBiblia juu ya maadili bora na utiifu wa mafundisho ya Kristo pamoja na ukweli kwamba siku moja tutatoa hesabu kwa matendo yetu, inashangaza kwamba tumewezakupiga hatua kidogo tu sana katika fadhila. Bado tunaonyesha sifa zinazohusishwa na jamii zisizo na habari; hivyo ni kusema ustawi hufanya moyo kuwa ngumu, nguvu na mamlaka zaidi kupindukia daima hutumika vibaya, tabia mbaya huchipuka tu zenyewe, ila fadhila, ikiwa inapatikana hata kidogo, ni kazi ya polepole na ngumu. Hata wana maadili hawafanyi kile wanachohubiri. Inaonekana kuwa ni sheria kwamba watu wako tayari kuteseka kutokana na athari mbaya za uovu kuliko kuchukua fursa za baraka za kuishi maisha ya utiifu wa Kikristo.
Iwapo twatafuta ushahidi zaidi kuhusu asili ya mwanadamu aliyeanguka, hatuhitaji kutazama mbali zaidi kuliko watoto wetu wenyewe. Hata wazazi wenye kanuni kali za Kikristo wanaweza kushuhudia jinsi ilivyo ngumu kujaribu kurekebisha watoto wetu wanapotukengeusha kwa mtazamo na matendo.
Mfano mwingine zaidi wa upotovu ni jinsi tunavyoweza kuchukua ukweli wa Biblia na kuitumia kwa njia mbaya. Kristo hudunishwa wakati wale wanaotumia jina lake wanalitumia kama udhuru wa ukatili au kutesa. Lazima tuwe waangalifu kiasi cha kuweza kutofautisha baina ya bidii iliyopotoka na kujitolea Kiukristo wa kweli. Historia inatoa mifano mingi sana ya watu waliojiita Wakristo lakini kwa kweli hawakuwa na upendo na fadhili za Kristo. Ni kana kwamba dawa inayoponya imegeuka na kuwa sumu ya kuua. Inasikitisha sana kwamba sisi ambao tunajitambulisha kama wafuasi wa Yesu, sisi ambao tuna heri ya kufunuliwa Neno la Mungu, sisi ambao tumefunuliwa ukweli wa asili ya Mungu, sisi ambao tunadai kwamba "ndani yake tunaishi na tunasonga mbele na "(Matendo 17:28), sisi ambao tunakubali upaji wake na baraka katika maisha yetu, na ambao tumekubali msamaha unaotolewa kupitia kifo cha Kristo msalabani, husahau mamlaka yake juu ya maisha yetu na kuwa baridi na kutomjali katika mioyo yetu.3
Labda ushuhuda bora kuhusu upotovu huu utatoka kwa wale ambao wanajitolea kwake Kristo kwa mioyo yao yote. Wanaweza shuhudia jinsi ilivyo ngumu kupigana na asili yao iliyoanguka wanapojaribu kuishi maisha ya uadilifu. Watakuambia kuwa kwa kutazama maisha yao wenyewe na jinsi akili zao zinavyofanya kazi, wamegundua hakika ya jinsi roho ya mwanadamu ilivyopotoka. Dhamira hii inazidi kukua kila siku. Watakuambia jinsi wanavyofanya vibaya katika imani yao, jinsi matamanio yao yamejawa na ubinafsi, na jinsi walivyodhaifu na walegefu wa moyo katika kujaribu kufanya jambo sahihi. Watakubali na kukiri kwamba mafundisho ya Kibiblia kuhusu asili hizi mbili za mwanadamu zinazopingana yamethibitika kuwa kweli katika maisha yao. Kwa maneno ya Paulo, "Nina hamu ya kufanya yaliyo mema, lakini siwezi kuyatimiza" (Warumi7: 18). Jinsi tu mtu alivyosema, hata hali ya kiroho tunayo pia imechafuliwa na asili yetu. Hatuna chochote cha kujivunia. Kinyume chake, inabidi kila wakati Mungu kwa neema avumilie makosa yetu na kwa rehema asamehe dhambi zetu.
Hii ndio hali halisi ya kiroho ya mwanadamu. Hakika ya maelezo na mkazo wake inaweza kuwa tofauti katika kila kisa, lakini kanuni za msingi zinabaki kuwa kweli. Tangu jadi au hata sasa, historia ya mwanadamu imekuwa rekodi wazi ya udhalimu wa kibinadamu. Huo ndio ukweli mchungu.
Tunapotazama uwezo ulio wa ajabu tunao sisi wanadamu, na kuulinganisha na yale tumewezakukamilisha nao, huwa ni ngumu kuelezea. Ni ngumu kupata maelezo ya kuridhisha. Maelezo ya pekee yanaonekana kuwa ni kwa kuwa mwanadamu amepoteza uhusiano wake na Mungu, basi kuna jambo la kimsingi linalokosa au lililombaya na kila mtu aliyezaliwa katika ulimwengu huu. Na matokeo yake ni kwamba, ijapo tuna uwezo wa kusema “La!” kwa tamaa ndogo ndogo, lakini tamaa hio bado imekuwa na nguvu ya kutosha kutuzidi hamu ya kufanya haki.
Tabia hii imesababisha upinzani katika asili yetu iliyoanguka tusijekujua ukweli juu ya Mungu. Wala hatutaki kujua kwamba kuna Mungu awekaye vigezo na matarajio ya maadili kwetu. Kadiri tunavyozidi kutenda dhambi, ndivyo ukweli huu unazidi kushamiri. Tumefungwa pingu za uovu ambazo zinatuzuia kutenda wema na kumtafuta Mungu. Kadri tunavyozama katika upumbavu huu, ndivyo tunavyokosakuelewa ukweli, na ndivyo moyo inazidi kuwa ngumu kumwitikia Mungu. Fikra zetu na dhamiri yetu mbovu zimepotoshwa hivi kwamba zinaongezea tu shida kwa kusababisha udanganyifu wa haki. Badala ya kuugua juu ya hali halisi ya maisha yetu, kwa kweli tunafikiria kila kitu kiko sawa nasi.
Hivi ndivyo dhambi hufanya kazi. Ni kweli kwamba kuna udhalilishaji zaidi au kidogo inayopatikana kati ya watu. Ni wazi kwamba wengine wanaishi utumwani. Ilhali wengine huonekana kuwa wameshinda shida hizo. Lakini ukweli unabaki kuwa hata ijapo haionekani kwa mtazamo wa nje wa mtu, lakini hio ndio hali ya kweli ya mioyo yetu sisi sote.
Ukweli huu umeenea sana hivi kwamba maelezo yake ya pekee lazima yatie nanga katika kasoro fulani ya hali ya kibinadamu. Kwa maana kutokukamilika huku ndiko kutaonekana kuwa ni maelezo ya kipekee ambayo yanaweza kuwajibikia ukweli huo. Huo sio tu uvumi bali ni ukweli ulio dhahiri ambao umedhibitishwa jinsi Bwana Isaac Newton alivyothibitisha nadharia zake za kisayansi kupitia majaribio na uchunguzi wa ukweli. Ndio nadharia ya kipekee ya asili ya mwanadamu ambao inaingiana na ushahidi wote.
Katika hatua hii, ni muhimu kugeuka na kuacha kutafuta visababu dhahiri au kufuatilia uchunguzi wa aina fulani, ili kuweza kuona kile Biblia inasema kuhusu hali hii. Biblia imejaa taarifa nyingi kuhusu asili ya mwanadamu aliyeanguka. Karibu katika kila ukurasa wa kitabu hicho tunapata thibitisho wa fundisho hili. Tunasoma maandiko kama vile, "Mawazo ya moyo wa mwanadamu ni maovu tangu ujana wake '' [Mwa. 8,21,]. "Je! Mwanadamu ni kitu gani, hata akawa safi? Huyo aliyezaliwa na mwanamke, hata awe na haki? '' [Ayubu 15,14]. Warumi Mlango wa 3 inasema kwamba wote wamefanya dhambi na wamepotea. Hakuna hata mtu mmoja mwenye haki. Tunaweza kuendelea na kuendelea: '' Moyo huwa mdanganyifu kuliko vitu vyote, na zaidi ya tiba. Nani awezaye kuujua? '' [Jer. 17: 9]. "Kwa kweli nilikuwa mdhambi tangu kuzaliwa, mdhambi tangu mamangu alipochukua mimba '' [Zab. 51, 5]. Kama Paulo, tunapaswa kulia, "Ole wangu, maskini mimi! Ni nani atakayeniokoa na mwili huu wa mauti? '' [Rom. 7:24]. Haishangazi kwamba Biblia husema kwamba mabadiliko kamili kwa asili ya mwanadamu inahitajika iwapotutaishi jinsi ambavyo Mungu alitukusudia tuishi.
Sehemu ya Pili: Dhana Potovu Kuhusu Uovu
Iwapo taswira ambayo Biblia hutupa kuhusu hali ya asili ya mwanadamu aliyeanguka sio mbaya ya kutosha, basi twahitaji pia kutazama jinsi shughuli za mapepo zinaendelea moyoni mwa mwanadamu aliyeanguka. Katika Biblia, Shetani anaitwa "mkuu wa ulimwengu huu" (Yohana 12: 31). Sasa hili ni eneo moja ambalo hutofautisha Ukristo wa kidesturi na imani halisi ya Biblia. Hata katika mataifa yanayodai kuamini katika Biblia, fundisho la uwepo na shughuli za shetani hukataliwa karibu kila pembe. Mara nyingi watu huvumilia Baadhi ya yale Biblia inafundisha, hata ijapo hio haijathibitishwa. Lakini suala la utu mbaya ni jambo lingine tofauti kabisa. Linachukuliwa kama hekaya za zama za kale. Tunapewa dhana kwamba ni somo ambalo mtu yeyote aliyeelimika huacha kuamini; kama vile ushirikina ambao unahusishwa na mizimu, uchawi na mapepo, ambayo inachukuliwa ni kama masalio ya nyakati za kutoelewa. Ni kweli kwamba fundisho hili la Kibiblia limepotoshwa sana. Wengine wanaimani mbovu ya kwamba taswira ya Shetani na marafiki wake kama vile wanyama wa kiroho wenye pembe na mikia ipo katika Biblia. Ama kweli kuzidi mwiongoni mwa waumini, wanaohusishwa na mawakala hawa, huwa ndio risasi inayodhoofisha ukweli wao.
Kwa hivyo, hii ni mada ambayo watu wanaweza kupuuza au kukejeli. Lakini hii inaonekana kuwa tofauti hasa kwa kuzingatia ukweli kwamba tunatambua uwepo wa watu waovu, waliopotoka katika fikira zao na matendo yao, ambao mara nyingi hufanikiwa kuwasawishi wanadamu wenzao kutenda dhambi na uovu. Mbona basi haishangazi kwamba kunauwezekano wa kuwa na viumbe vya kiroho vya aina hizi ambavyo huwajaribu watu kutenda dhambi? Ni hio dhana tu ambao watu wameshikilia kwamba viumbe vile haviwezi kuweko ndiyo inawazuia kuona mkengeuko katika msimamo wao. Hawaamini katu kile kinachofundishwa na Biblia kuhusu jambo hili.
Kwa wale ambao wanaamini, hili ni swala nyeti. Linatuwezesha kutambua ni katika vita gani hivyo tunashiriki. Tunao dosari ndani yetu na vile vile nje tunajaribiwa. Je! Tunao tumaini lolote? Tunaposoma kwa mara ya kwanza yale Biblia inasema juu ya Mungu, inafanya hali yetu kuonekana tu isiyokuwa na tumaini lolote. Tunaambiwa kwamba hatuwezi kumficha Mungu chochote. Anajua tunachofanya, na anajua hata na yale tunayofikiria. Anajua yaliyo mioyoni mwetu. Anaona hata na giza la ndani kabisa.
Pamoja na hayo ongezea yale ambayo Biblia inasema kuhusu hukumu ya Mungu na yale tunajifunza kutokana na tendo lake la kuwalipiza kisasi wana wa Israeli. Kuanzia Sodoma na Gomora hadi Ninawi na Babeli, tunamwona Mungu akihukumu dhambi ya mwanadamu. Hata ingawa tunafahamu machache juu ya wema wa Mungu, lakini ile mifano tunayosoma lazima itusababishie wasiwasi kufuatia kushindwa kwetu kuishi kulingana na maagizo aliotoa Mungu. Na je!
Tutafanya je na vifungu kama hizi?-
Kwa kuwa nimeita, nanyi mkakataa;
Nimeunyosha mkono wangu, asiangalie mtu;
Bali mmebatilisha ushauri langu, wala hamkutaka maonyo yangu;
Mimi name nitacheka siku ya msiba wenu;
Nitadhihaki hofu yenu ifikapo;
Hofu yenu ifikapo kama tufani,
Na msiba wenu ufikapo kama kisulisuli,
Dhiki na taabu zitakapowafikia.
Ndipo watakaponiita, lakini sitaitika;
Watanitafuta kwa bidi, wasinione. Kwa kuwa walichukia maarifa,
Wala hawakuchagua kumcha
BWANA. (Mithali 1: 24-29).
Kusema kwamba hii ni lugha nzito haitoshi. Sio kwamba Biblia inahitaji uthibitisho, lakini ulimwengu unaotuzunguka unaonyesha wazi kwamba kuna aina ya kupanda na kuvuna ambayo inathibitisha kwamba kupuuza yale ambayo Biblia inafundisha kuna asili yake ya uharibifu. Dhambi ina matokeo. Tunaona matokeo hayo kote karibu nasi.
Na ikiwa yote haya ni kweli, basi yatupasa kufanya nini? Kunao tumaini lolote? Je! Hukumu ndio itakua hatima yetu pekee? Kwa shukrani, kuna tumaini. Tunapokuja kutambua hali halisi ya maisha yetu, tunakua tayari kabisa kuthamini kile ambacho Mungu amefanya ili kutuokoa kutokana na nafsi zetu. Ni muhimu kwamba tuchukue kwa uzito asili yetu ya wanadamu walioanguka. Bila ufahamu na utambuzi huu, hatutakuwa na msingi wa kutosha ambao unaweza kujenga imani halisi. Hili sio swala la maneno matupu tu ya kitheolojia; lakini ni suala la vitendo. Wakati hatuchukui shida yetu kwa uzito, hatutafuti suluhisho ambayo Mungu hutoa na kiwango cha ukweli na nguvu ambayo hali yetu ya kweli inahitaji. Ikiwa hatuelewi jinsi sisi tu wagonjwa sana, hatutafuti tiba kwa bidii inayohitajika. Na iwapo twaugua kidogo, tunachukua aspirini. Lakini iwapo hali yetu ni maututi, twafuata tiba kwa shauku kabisa. Sasa tiba hiyo sio ya kulazimishwa kwetu; bali ni ofa imetolewa kwetu.4
Ni faida kubwa kuelewa jinsi tunavyo kasoro. Hutusaidia kuondoa udanganyifu na ukawaida wa kiroho. Ni kutokupenda uwazi na uaminifu tu ndio kunaweza tuzuia kuhitimisha kwamba sababu na uzoefu zinatuambia kwamba yale ambayo Biblia inasema kutuhusu ni kweli. Hatuna udhuru iwapo tutabaki kuyakataa.
Hatupaswi kubaliana tu na ufahamu huu, bali pia ni lazima tuhisi ukweli huo kwa kuipitia maishani. Tunapoona karibu nasi athari ya kutokuchukulia ukweli huu kwa umuhimu unaofaa, na kupitia ukali wake maishani mwetu, tunakuwa na msimamo dhabiti wa kusonga mbele katika maendeleo yetu ya kiroho. Na vile vile tutakuwa na mtazamo tofauti kwa wale ambao dhahiri wanapambana katika maeneo ambayo labda tunaweza kuwa na shida kisiri. Siku kwa siku ufahamu wa hali yetu utatusaidia kukua kiroho.
Sehemu ya tatu: Makataa ya Kweli Hizi
Pamoja na hayo yote yaliyosemwa, bado hatujakabili shida yetu kuu: Kiburi haipendi kuwa mnyenyekevu. Wakati ukweli unamkabili, mtu mwenye kiburi hujaribu kumlaumu Mungu. Lakini kando na yote, kuna hoja huja kwamba, ni nani aliyetuumba? Sasa mtu mwenye kiburi atafikiri kwamba hii, kwa njia fulani, humwondolea hatia ya dhambi. Anafikiria kwamba Mungu hatamhitaji kuwajibikia vigezo ambavyo yeye, kwa asili yake, anadai kuwa hawezi kuzishika. Sasa hoja ya mizunguko isioeleweka wa namna hii haina maana.
Tukichunguza hoja hii wakati wasioamini wanaitumia, tunapata mambo mengine tofauti. Hata ijapo tutawaonyesha dosari kwenye fikira zao, bado haimaanishi kwamba watakuwa wazi kwa ujumbe wa Biblia. Ikiwa tunaweza tu kuwashirikisha wake hawa na waume hawa katika mazungumzo ya kweli, tunaweza kuwa na nafasi nzuri ya kuwasiliana kwa kutumia hoja thabiti kwa manufaa ya imani ya Kikristo ambayo hata wasomi zaidi wamethibitisha. Iwapo tutaweza kuelezea Ukristo kisawasawa, basi dhana pingamizi ya hapo awali itakuwa athari ndogo katika maoni yao.
Anza na mambo ya kimsingi kabla ya kupanda kiwango cha kujaribu kuelezea mawazo ya Mungu isiyowezekana kuelezea. Ni maoni yangu kwamba hii ndiyo njia bora ya kuwafikia wale ambao hawajaamini. Ni muhimu kujua kwamba ninazungumzia kurasa hizi kwa wale ambao tiyari wanadai wamekumbatia imani ya Kikristo. Kwa wale ambao wanakubali wema na haki ya Mungu na hali asili ya mwanadamu, mwisho huo sio kisingizio cha kutosha kuelezea dhambi za mwanadamu. Tunawajibu, hatuna udhuru.
Biblia inasema wazi kuwa dhambi haiwezi kulaumiwa kwa jinsi Mungu alivyotuumba. "Unapojaribiwa, hakuna mtu anayepaswa kusema, 'Mungu ananijaribu' '(Yakobo 1:13). Mungu anataka tuafikiliane na dhambi zetu na tugundue suluhisho Alilotoa ambalo linaweza kutuokoa kutoka kwa hukumu.
Tunaporuhusu tabia zetu na kuifanya kwa kuegemea theolojia, tunaweka hatua dhabiti ya msiba. Sote tunawajibika: Asili yetu iliyoanguka sio udhuru. Tunawajibika: Mungu sio wa kulaumiwa. Hatia tunao na tunastahili hukumu. Mafundisho mengine yoyote hayo hupunguza na inakanusha umuhimu wa ukweli wa msalaba wa Kristo. Yote tisa, kumi ni kwamba: Hali yetu ya asili ni dhaifu na imeanguka na majaribu yetu ni mengi; Mungu ni Mtakatifu kabisa, lakini Yeye hutoa msamaha, neema na uwezeshaji kwa wale ambao ni waaminifu kwake na wako tayari kutubu.
Hii inaweza kuwa si rahisi kuelewa. Maisha ni nini? Siri za anga za juu zinatosha kutukumbusha juu ya upungufu wetu na kufanya unyenyekevu ndani yetu. Je! Inashangaza kwamba hatuwezi kuelewa kikamilifu huyu Mungu asiye na kipimo? Na ingawa mambo kadhaa juu ya imani ya Kikristo ni ngumu kuelewa, kweli za kimsingi ziko wazi. Mambo mengine Mungu amefunua; ila mengine yamebaki kuwa siri. Hivyo tuangalie yale tunayojua, sio yale ambayo hatuwezi kuelewa.
Kwa sisi ambao tumejua kuwa maisha inatuanda kwa umilele, tunapata wakati mgumu kuelewa mtu ambaye anaendelea kutawaliwa na ujanja ndogo ndogo na kiburi huku akipuuza habari yote njema ya Yesu Kristo. Ni kama kuja mbele ya hakimu mahakamani kwa mastaka ya hatia ilio wazi unao na hapo,jaji anapo kupa njia ya kuzuia adhabu, unageuka na kujaribu kumlaumu jaji kwa kile kilichotendeka. Hiyo itakuwa upumbavu kupindukia! Tunapozingatia yote haya, tunakuja kufahamu kile alichoandika John Milton:
Je! Ni nini bora zaidi tunaweza kufanya, kuliko kusujudu mbele yake kwa heshima; na kukiri kwa unyenyekevu makosa yetu, na kuomba msameha; Kwa machozi inayomwagika ardhini, na kwa kuugua kwa
Mara kwa mara, inayotoka ndani ya mioyo uliovunjika, kama ishara ya kuuzunika kusiyozimika , na unyenyekevu wa kudhalilisha? 5
Vidokezo
1. John Milton, Paradise Lost, bk. 1, mistari 91-92
2. Wilberforce hapa ananukuu Historia ya William Robertson ya Amerika. Itakumbukwa kwamba Waingereza hawakuwa wanapenda Amerika kwa wakati huu. Mnamo 1797, mwaka wa kuchapishwa kwa kitabu cha Wilberforce, George Washington alikuwa anamaliza kipindi chake cha pili kama rais na Mfalme George III alikuwa bado kwenye kiti cha enzi cha England. Wilberforce mwenyewe alikuwa amepinga upinzani wa England dhidi ya koloni na alikuwa rafiki ya Wamarekani wengi, pamoja na Benjamin Franklin.
3. Wilberforce hapa anataja mifano katika historia ambapo uovu mkubwa umefanywa kwa jina la Kristo. Labda alikuwa akifikiria hafla kama mauaji ya wanawake wasio na hatia na watoto wakati wa Vita vya Makumbusho au uovu wa uchunguzi wa mahojiano, ambapo wahasiriwa wengi waliteswa kikatili na kuuawa kwa jina la Kristo.
4. Wilberforce huhariri maneno haya katika maandishi ya asili.
5. Milton, Paradise Lost, bk. 10, 1086-92.