SURA YA TANO
SURA YA TANO
HOJA ZA UKRISTO WA KWELI
Ubora wa Imani Halisi ya Kikristo, Ushahidi wa Asili Yake Takatifu
Wacha nikaende kando kidogo na mpango wa hatua amabao nimekuwa nikifuatilia kuonyesha viwango kadhaa vya Ukristo ambavyo napata kuwa ni sehemu ya uzuri wa imani halisi. Ukristo wa kidesturi hauna manufaa hizi, na wale walio Wakristo wa kidesturi hawana hata wazo duni la kile ninachonuia kusema. Ingawa ninatelekeza mpango wangu wa hapo awali, natumai kwamba utakapoelewa kile nakaribia kueleza, utaona jinsi haya makala yanavyohusisha yote nimekwishaandika mpaka sasa.
Ni kweli kwamba hata uchunguzi wa haraka haraka wa imani ya Kikristo unaonyesha mambo ya ajabu ambayo Mungu amefanya ili kuonyesha upendo wake. Lakini tunapochukua muda na juhudi za kuchunguza kwa makini maajabu ya imani ya kweli, tunaona hata zaidi uzuri wa mfumo huo. Hebu na nirejelee somo la mlango wa mwisho kwa dakika ili kuonyesha kile ninachozungumzia. Hapo tuliona jinsi mafundisho ya msingi ya Biblia na ushawishi ambao mambo hayo yako nayo katika maisha yetu yalivyo katika maelewano kamili hivi kwamba mtazamo wa kawaida wa imani hushindwa kushikilia.
Labda sihitaji kutaja, lakini nitataja, kwamba uwiano huo mkamilifu upo kati ya mambo mbalimbali ya imani ya kweli ya kibiblia. Uwiano huanza na ukweli wa msingi wa asili yetu ya binadamu iliyoanguka, uhusiano wa kupatanishwa na Mungu ambao kazi ya Kristo juu ya msalaba hutupa, na urejesho na mabadiliko ya utu wetu wa ndani kwa uwepo na matendo ya Roho Mtakatifu. Yote tatu hayo ni sehemu ya moja inayodumu katika umoja na kuheshimiana.
Jinsi hii ilivyo kweli na misingi ya imani, pia ndivyo ilivyo na mafundisho yote yaliyo mbele kuhusu imani ya Kikristo. Yote yanaenda pamoja katika uwiano wa ajabu ambao unaunda msingi wa maisha ya maana, wakati wa sasa na katika wakati ujao.
Matendo na kufikiri zaidi kunaosisitizwa katika Biblia kama lengo la maisha ya kiroho ni heshima na kumpenda Mungu; upendo, wema, na upole, kwa wanadamu wenzetu; zingatio sahihi kuhusu mali na matukio ya maisha haya ikilinganishwa na vitu vya milele; na tabia njema ya kujikana nafsi na unyenyekevu.
Tayari nimeelezea uhusiano kati ya mitazamo na moyo wetu kwa Mungu na jinsi hii kuathiri mitazamo na tabia zetu kwa watu wengine. Hasa, unapochunguza kwa karibu jinsi baadhi ya viwango vya tabia yako hufanya kazi pamoja ili kukuza na kuimarishana moja kwa mwingine, hauna lingine ila kufikia hitimisho kwamba zipo na zinafanya kazi katika uwiano kamili. Hii inaweza kutambuliwa kutokana na kile ambacho tayari kimeandikwa, lakini ningependa kutazama kwa haraka uhusiano huu. Kwa mfano, unapochunguza vitendo vya wema na unyenyekevu, utaona kwamba msingi kamili ambao kwao tabia hizi hutokea ni fadhila ya kujikana nafsi na kiasi katika kufurahia mali yako.
Sababu kuu inayofanya watu wasiweze kuwasiliana pamoja ni kwamba wengi wao wamejawa na kiburi na hali ya kupotosha ya kujiona u muhimu. Hii huwasababisha kuhitaji wengine wawaone jinsi wanavyojiona wenyewe na huelekeza kwa tathmini isiyo ya kweli ya thamani ya mali na heshima ya kidunia. Mienendo hii husababisha mashindano ya kutisha kati ya waume na wake ili kuimiliki. Ncha mbaya ya mtu mmoja husuguana nay a yule mwingine na kujenga mkuarusano ambao utavuruga utulivu baina ya mtu na mwingine na pia kuvuruga amani.
Kristo anapokuwa kazini katika maisha yetu, yeye hulainisha ncha hizi mbaya. Badala ya kukuarusana mmoja kwa mwingine, tunafanya kazi pamoja kama mashine iliyotiwa mafuta vyema kwenye viungo. Huu unapokuwa sivyo, tunapaswa kushangaa kama tunaona Ukristo wa kidesturi badala ya imani ya kweli. Wakristo wa kidesturi wanaweza wanaweza kusema kuwa kunahitajika upendo na ukarimu, lakini utumwa wao wa kiburi na kujiona muhimu huwaongoza kutokana na kutekeleza maadili haya na kuwaongoza katika kutafuta mafanikio ya kibinafsi na ya kitaaluma.
Wengine wamepata muonekano wa nje ambao huwawezesha kufuata malengo haya wakati wa kudumisha wema, lakini wanakosa upendo wowote wa kweli katika mioyo yao. Wakati shinikizo ni juu, hata kama ni kwa njia ya tamaa au mng’ang’ano wa kibinafsi, rangi yao ya kweli itaonekana. Hata wanaweza kuwa wanajua kuficha ukatili wao, lakini kwa ndani wanatokota. Hasira yao inaweza kulipuka dakika yoyote iwapo watashindwa kujizuia. Hii inaonekana kuwa ni kweli hasa kwa wale ambao wameinuliwa na mafanikio ya jamii yetu au kwa udanganyifu. Wamejifunza jinsi ya kuweka sura ya utu wema na heshima wanapofuatilia maslahi yao wenyewe ya ubinafsi. Ni kama watu wamekaa kwenye meza ya karata. Wanaweza kuonyesha mtazamo mzuri kwa wengine kwenye meza, lakini ndani yao wanatarajia wengine watapoteza ili wapate kushinda. Ni namna ya kujifanya unaokuacha ukiwatamani wake kwa waume wa madaraja ya kazi ambao kamwe hawakuwa na nafasi ya kujifunza kile kinachojulikana kama tabia na ambao wanakuruhusu kujua hasa kilicho akilini mwao.
Imani halisi haina haja na kufunika uso na fadhila bandia. Inahitaji ukweli katika utu wa ndani. Mtu wa Imani husimama mbele ya Yule anayechunguza mioyo yetu (ona Zaburi 139:1-4). Muumini wa kweli hujaribu kuishi katika mazingira ya wema naye anafanya kila juhudi kukwepa tendo lolote au wazo lolote ambalo litachafua au kuharibu usafi wake. Hii ndiyo sababu kujiweka katika nafasi ambapo tunashindana kuinuka juu ya wengine inaweza kuwa na madhara makubwa sana kwetu. Ni vigumu kumpenda mtu kwa dhati wakati juhudi zako zote ni kuinuka juu zaidi yake.
Maagizo ya Biblia yanayotuagiza kuweka mali na heshima katika mahala pao kamili yanasaidia kutuweka huru ili kupenda. Yanatuwezesha kuwajali kikamilifu wale ambao wamekuwa na fanaka zaidi kulingana na viwango vya ulimwengu, hata ijapowalikwisha jaribu kutuzuia tusifanikiwe na sisi. Tunapo weka “mawazo yetu kwa vitu vilivyo juu” ( Kol. 3:2) hatuna sababu ya kuona wivu au kuwa wakali na ambao malengo yao yapo kwenye mali na umarufu wa kilimwengu.
Maagizo ya imani halisi ya kutozingatia sana jinsi watu wanavyotuona vile vile yanatuweka huru kuwapenda hata na wale walipotuvamia ama kudunisha hadhi yetu. Kipimo bora ya uhalisia wa imani yetu ni jinsi tunavyo jibu wale wanaotuvamia na kututenda ni kana kwamba wako zaidi yetu. Unyenyekevu wa kweli hushughulikia mambo kama hayo kwa neema. Tusipowalipiza kisasi wanaotukosea, tunafungua mlango wa mapatano kati yetu na wakosefu wetu.
Ni fadhila nyingine ya imani halisi kwamba fanaka ya kimaadili inachukuliwa kuwa wa thamani zaidi ya masomo. Hivyo yahitajika kuwa waumini watafute zaidi kufaulu kimaadili kuliko maarifa. Sasa hii ni kinyume na wale wanojulikana kama madhehebu ya kimafumbo yanaoelekeza wafuasi wao kwa kile kinachojulikana kama maarifa ya ndani ambayo huwa ndiyo chanzo cha wokovu wao.
Unapotazama mengi ya dini kubwa ulimweni, kama vile Uhindu au Uislamu, utapata matabaka tofauti au viwango vya maendeleo kulingana na kiasi cha taarifa ambayo mtu anayo. Ni wazi kwamba hii inaweka wale walio katika matabaka ya chini, ambao wanaweza kuwa na uwezo wa kusoma, katika hasara kubwa. Wengi hawawezi kamwe kufanya maendeleo zaidi katika mifumo hii. Baadhi ya wanafalsafa wa kale hata wanawezatetea kwamba kudumisha watu katika jinga ni kwa manufaa ya jamii. Hii inaashiria kwamba wengi wa wanadamu ni kizazi duni kulingana na wasomi wa juu, wenye elimu zaidi. Ukristo wa kweli unafanya kazi kwa njia halisi. Sio tu injili inayolenga kwa wanadamu wote, bali pia ina sehemu maalum miongoni mwa maskini. Ilikuwa hata sifa na Yesu kama "habari njema kuhubiriwa kwa maskini" (Luka 7:22).
Mkazo ambao Ukristo wa kweli unaweka juu ya upendeleo wa fadhila za kimaadili juu ya mafanikio ya kimasomo ina thamani ambayo inapita namna ambavyo wema unaofaa malengo ya imani. Ni lengo ambalo kwalo tuna uwezo wa kufaulu vyema. Sio sisi sote tuna uwezo wa kufikia ukuu kimasomo, lakini sote tunaweza kufanya vyema zaidi katika kutafuta wema. Wale ambao wameshafanya kupata elimu kuwa shauku yao ya kawaida ndiyo wa kwanza kutambua kwamba mafanikio yao yamekuwa ya wastani tu kwa bora. Hata kama watu hawa sio wazi bayana, bado tutapata ushahidi wa ukweli huu wenyewe. Ni miongoni mwa safu zao kwamba tunapata mifano mbalimbali ya udhaifu, maono duni na tabia ya kufanya makosa. Waadilifu zaidi na wasomi zaidi ni wale wanaotambua ubatili wa fahari yoyote katika hekima ya mwanadamu. Kwa kawaida ni wasomi wa bandia ambao wanacheza mchezo huo na kujificha nyuma ya taswira hii bandia.
Hali haiwi hivi katika harakati za kutafuta uadilifu. Wanadamu waliumbwa kwa mfano wa Mungu. Ingawa tumeanguka na sura hio imeshaharibika, bado kuna sehemu ya sura ya Muumba katika kila binadamu. Ni sehemu ya maumbile yetu ambayo inaweza badilishwa tena ikafanane na Kristo (ona Efe. 2). Kwa sababu ya Kristo tuna njia zilizopo, sio tu kusamehewa, bali pia kusafishwa na kufanywa upya katika hali yetu ya ndani. Kwa uwepo wa Kristo ndani kwa njia ya Roho Mtakatifu, tumeendelea kuwa na uwezo wa kujitahidi kupata maendeleo halisi katika juhudi zetu za kuishi maisha ya kweli ya Kikristo. Tunapochukua fursa ambayo Mungu ametoa ili kukabiliana na harakati hii, tunaweza kuwa na imani kwamba atatusaidia kufaulu.
Nimeshajua wanaume na wanawake ambao walikuwa na mifano ya maisha ya ukweli huu. Acha niwaambie kuhusu rafiki mmoja ambaye alikuwa mfano mkubwa kwangu katika eneo hili. 1 Hakuishi maisha marefu, lakini ilikuwa ni moja iliyojaa kazi kubwa. Alifanya dunia mahali pazuri kupitia maisha yake. Mfano wake ni motisha kwa wote waliomjua kuwa ana bidii katika kutafuta maisha kama hayo yake. Natumai hudhani kwamba navichukua hivyo vipawa vingine Mungu ametupa au matokeo ya juhudi za kibinadamu katika maeneo hayo mengine kijuu juu tu. Lakini katika uaminifu wote, inapolinganishwa na ile taswira kuu na utukufu wa Mungu, sifa ya mafanikio ya kibinadamu yote ni kama sifa zile tunazompa siafu kwa ajili ya mzigo ule anaoweza kubeba ikilinganishwa na uzito wa mwili wake. Kazi kama hiyo inaweza kuonekana kuwa ya kushangaza, lakini haina athari kubwa kwa ulimwengu ambamo tunaishi. Hiyo ndiyo ubatili yetu. Mafanikio yetu binafsi inapewa thamani ya juu sana kupita kiasi. Hivi sivyo hali katika kutafuta heshima yetu ya kweli.
Pia ningependa kutaja kwamba sijaribu kutoa ushahidi wa ukweli wa imani ya Kikristo. Wengine walio na sifa nyingi kuniliko tayari wameshafanya vya kupendeza katika kazi hiyo. Waandishi kama vile William Paley wanastahili sana shukrani kwa jinsi walivyochukua ushahidi kwa niaba ya imani ya Kikristo kuonyesha kwa ustadi mkubwa namna ilivyo ya maana sana.2 Nikishasema hivi, ningependa kutaja mojawapo ya vitambulisho vya imani hio kinacho nivutia kwa njia fulani. Hii ndiyo njia ambayo mito mingi ya msaada huja pamoja ili kuunda kisa. Idadi kubwa ya waandishi wameandika aina na aina ya ushahidi ambao unaunga mkono madai ya Kristo na Ukristo. Wamechunguza ushahidi kutoka kwa unabii, kutoka kwa miujiza, kutoka kwa tabia ya Kristo, kutoka kwa asili na ubora wa maagizo ya vitendo vya imani na kutoka kwa njia ya ajabu mafundisho ya imani yanayoichochea vitendo vya imani. Wengine wamechunguza kwa makini ushahidi wa ndani wa Biblia wenyewe, pamoja na ushahidi wa awali wa ukweli wa imani katika maisha ya wale ambao walitangaza.
Kuna mistari mingi ya hoja ambayo imekuwa toleo katika kutetea imani. Wingi wa ushahidi hufanya hoja dhidi ya Ukristo kuonekana kuwa isiyo na maana. Kwa hiyo, mistari mingi tofauti ya ushahidi, yote yenye nguvu, inayokuja pamoja ili kuimarisha uaminifu wa Ukristo, hauwezi kuelezewa isipokuwa kwa mantiki ya ukweli wake. Siamini kuwa unaweza kuchunguza mfumo mwingine wa dini ulimwenguni kwa wingi wa mbinu na kupata ulinganifu na uwazi unaopata katika Ukristo wa kweli.
Vidokezo
1. Wilberforce pengine anazungumzia rafiki yake Matthew Babayo, ambaye hivi karibuni alifariki.
2. William Paley alikuwa ni mtetezi mzuri wa Ukristo katika siku hizo za Wilberforce.