USHAURI WA PETRO KWA WAZEE
R5185 Saint Peter’s Exhortation to the Elders
USHAURI WA PETRO KWA WAZEE
“Nyenyekeeni chini ya mkono wa Mungu ulio hodari, ili awakweze kwa wakati wake” – 1 Petro 5:6
Kama wale ambao wamepokea neema ya Mungu na ujuzi wa kusudi la Mungu, watu wa Bwana wana tamaa fulani ambayo ni sawa na Sahihi, na ambayo inapaswa kutumiwa vizuri, kuthibitiwa na kuongozwa. Hakuna mtu anayepaswa kuwa na tamaa ya ukuu isiyofaa. Hatuwezi kufikiria Mungu bila tamaa. Wale ambao wana kiasi kidogo au hawana hupitisha maisha yao katika hali ya kutoeleweka wakijikamilishia kiasi kidogo sana kwao wenyewe na kwa wengine, na kwa kawaida hushindwa kutekeleza lolote.
Kuna, hata hivyo, matarajio ya kiungwana na ya upumbavu. Watu wengine wanatamani kuwa wasifika, wanaojulikana; wengine wanatamaani kutawala; bado wengine wanatamaani kuwa wakwasi, kutajika kijamii, au kwa majina na heshima kati ya binadamu. Haya ni matarajio ya ubinafsi, lakini ni nguvu ambayo inatikisa dunia hivi leo – katika miradi ya biashara, kijamii, kisiasa na hata kidini. Haya ni matarajio mabaya; na ingawa hayawezi kutumbukia katika uovu, lakini wote wana ubinafsi, na wanaelekea katika uovu. Wengi wanashawishika kwa matarajio ya ubinafsi katika kufanya mambo ambayo dhamira yao haiwezi kuruhusu.
Mkristo amejiwekea mbele yake tamaa kubwa zaidi iwezekanavyo. Mungu anawaita watu kutoka ulimwenguni kwa ajili ya Jina Lake. Kabla ya haya ameweka matarajio makubwa.
Hawa wamealikwa warithi pamoja na Yesu Kristo Bwana wetu. Hii ni tamaa ambayo inawahamasisha kuendeleza sifa zote za juu za akili na tabia, ili kujiandaa wenyewe kwa ajili ya jamii, urafiki na ushirika wa Baba wa mbinguni na Bwana. Hebu tuwe na matarajio hayo ya juu mbele yetu, kama motisha kwa wale wanaotegemea kutii Neno la Bwana
Wale ambao wanachukua mwenendo huu wanampendeza Baba. Ana kazi nyingi za kutekeleza na anawatafuta watu watakaofanya hayo. Yesu Kristo ni kichwa cha kazi hii kubwa, na ufalme wake ni kutawala na kubariki ulimwengu na walimwengu, hayo katika ulimwengu ujao, Mungu anaweza kuonyesha utajiri wa neema na ukarimu wake kwetu sisi (Waefeso 2: 7). Wale wanaothamini wito huu wa juu wanataka wawe na Mungu mahali ambapo amewaalika wawe. Wale ambao hawajali kile ambacho Mungu ametoa au ambao hawataki kuzingatia masharti wasijitose mbioni kwa ajili ya tuzo hiyo.
Wale walio na matarajio ya mbinguni wasihofu kitu na wasisahau kuwa wana hazina ndani ya maumbile katika vyombo vya udongo. Kwa tabaka hili inakuwa tamaa isiyofaa kutumikiana na kujengana katika imani iliyo takatifu. Bibi Arusi ajiweke tayari (Ufunuo 19:7). Watafute namna ya kuwa tayari wenyewe na kuwasaidia wengine ambao ni wa familia ya Mungu.
HATARI INAYOHUSIKA KATIKA HUDUMA YA WAZEE
Kutaka kazi ya askofu, mchungaji, ni tamaa nzuri (1 Tim 3:1). Ikiwa mtu anashughulikia mambo ya uchungaji wa kundi, hawezi kuwa na wakati wa maslahi mengine. Wale ambao wameitwa kwa nafasi ya wazee kati ya watu wa bwana, na wanapaswa kuwa makini sana kutafuta, si kwa ajili ya fedha ovyo, lakini kwa akili tambuzi (1 Petro 5:1-4). Lakini katika kutafuta nafasi hii basi kila mmoja akumbuke kwamba kuna hatari ya kuwa na kiburi na kujitakia nguvu na ukubwa. Wale walio na fursa ya kuhudumu kama ndugu mzee lazima waangalie ya kwamba hawaweki mizigo juu ya urithi wa Mungu. Wanapaswa kukumbuka kwamba wao si Mchungaji Mkuu. Ikiwa yeyote anapaswa kujisifu juu ya kundi; anaweza kujiumiza yeye mwenyewe na hata kanisa; kwa kufanya hivyo atakuwa anaendeleza moyo wa kiburi.
Petro anatwambia ya kwamba “Mungu huwapinga wenye kiburi, lakini huwapa wanyenyekevu neema” (1 Petro 5:5). Kwa hiyo ikiwa katika huduma ya Bwana mtu ni mnyenyekevu, mwenendo wake sio tu kwa faida ya darasa, lakini ndiyo njia pekee ambayo mtu yeyote atapata nafasi katika Ufalme. Uzee ni kazi ya heshima inayoweza kuleta matarajio mema na makuu na pia yaweza kuwa sababu ya majaribio makuu na hatari kuu. Yakobo anasema: “Ndugu zangu, msiwe waalimu wengi (kati yenu) mkijua ya kuwa mtapata hukumu kubwa zaidi (Yakobo 3:1).
Mtume anawahimiza wale ambao ni wazee wanaofanya kazi hiyo, “Basi nyenyekeeni chini ya mkono wa Mungu ulio hodari.” Kila kitu kinafanyika kwa nguvu za Mungu, ambayo kwayo husababisha vitu vyote kufanya kazi kwa pamoja ili kupata mema. Hatuwezi kuingilia kati mapenzi ya Mungu. Tunaweza kuruhusu kiburi na tamaa kali kuzuia maendeleo, lakini hatuwezi kuzuia mpango wa Mungu.
Sisi sote tunataka kutafuta njia bora ya kuwahudumia wengine na mwishowe kupata dhawabu kubwa. Petro anatuonyesha hiyo njia: - “Nyenyekeeni ” Kama Malenga alivyotuchorea:
“Naogopa kugusa
Vitu vinavyohusisha mambo mengi. ”
Roho itatufanya tuwe na hofu sana ya kuendeleza kiburi au ukuu au tamaa ya kuwanyanyasa wengine. Kwa hivyo tunajinyenyekea na kukumbuka kuwa Mungu atawabariki hasa wale walio wapole, waaminifu zaidi, na muda sio mrefu atawainua – wakati wa kuja mara ya pili kwa Bwana wetu.
Wakati mwingine, kusema kweli, wale walio wapole kati ya watu wa Bwana wanaweza kukosa kutambuliwa katika kanisa kuliko wale wasio na kipaji hiki cha tabia. Kuna tabia ya mwanadamu inayoelekea kinyume. Wangependa kuwa na mtu anayewanyanyasa kuliko yule ambaye ni mpole na wa moyo wa kiasi. Kwa hivyo wanaweza kukosa kutupenda. Lakini hatupaswi kutafuta kile kinachoweza kupendwa ndani yetu. Lakini tukumbuke ya kuwa twafaa kumtumikia Bwana kwa njia zake, na ya kuwa wajibu wetu mkuu mbele zake Bwana ni kwa faida yetu sisi wenyewe. Tunyenyekee chini ya mkono hodari wa Mungu ili tupate kuinuliwa wakati unaofaa.
KUNA HATARI KATIKA KUWA NA UJUZI MWINGI WA UKWELI
Haya mambo yote yaonyesha kuwa mtazamo wetu sahihi uwe wa unyenyekevu. Mawazo ya mioyo yetu yasiwe yale ya kiburi, bali yawe ya upole, uaminifu.
Kiburi ni uchoyo uliozalisha mbegu mbaya. Roho ya ubinafsi hujikusanyia kwa ulafi vitu vingi iwezekanavyo avionavyo kuwa vizuri na vyenye thamani – mali, elimu, heshima, jina kuu na sifa mbele ya binadamu. Kipimo cha mafanikio katika kujikusanyia hazina hizi husababisha hali ya uchoyo na hali ya kukata tamaa, uhuru na kutojali maslahi ya wengine. Roho ya namna hii, hatua kwa hatua huendeleza kiburi kwa haraka, kiburi cha kujitegemea, kitaendelea kuiva kwa kupata mafanikio yoyote yale. Na ubinafsi unavyozidi kuiva hujitokeza kwa uwiano wa ujinga na kujifurahisha kwa kujibeba, na kujisifia umaarufu wa kufikirika tu na heshima na sifa.
Hekima na unyenyekevu ndizo njia nyepesi zaidi. Moyo wa unyenyekevu hautafuti mambo yake tu, haujivuni, haujaribu kujikusanyia makuu, haufikiri mambo ya juu kuliko kipimo, bali hufikiria kwa upole – pasi na kupandisha sana au kushusha sana hali yao ya walichopata au walichofaulu kuwa nacho. Unyenyekevu hujaribu kila mara kufanya kazi kwa msingi imara, ingawa inasisitiza kuwa uaminifu kupata uhalali halisi na kufikia utukufu wa kweli wa kusifu na kupenda.
Kuna nafasi kwa sehemu ya watu wengi wanaopendelea kujivuna kwa sababu ya ukweli, kana kwamba tulikuwa tumeutunga ukweli. Ujinga ulioje! Hatujaanzisha ukweli wowote. Tulichofanya ni kutupilia mbali baadhi ya makosa yaliyotuziba macho hapo awali. Ukweli ni wa Mungu. Ameturuhusu kuona nje ya giza kuu ya kutokujua na ushirikina katika ukweli wa mpango wake. Kama kuna mtu aliyewahi kuona picha maridadi halafu ajivune kama ndiye aliyeichora, tungeweza kusema, “Mtu Mpumbavu! Hukuunda picha hiyo. Ulichofanya ni kuangalia tu. Hapana cha kujivunia hapo. ”
Hatushiriki katika kuunda sehemu yoyote ya mpango wa Mungu wa Zama. Kama tungejaribu kufanya hivyo, tungeshindwa vibaya. Akili yetu basi, inapaswa kuwa, “Njoo, tutawaonyesheni kile ambacho Mungu amepanga, kile Mungu amechora.” Hivyo tungempa Mungu utukufu na kuwa wa msaada kwa wengine; maana tunapoonyesha mfano wowote wa kiburi na ubinafsi katika ukweli kwa kiwango hicho tunajiumiza na kuwaumiza wengine. Ulimwengu waweza kusema, “Tuna madaktari wa mambo ya Mungu katika madhehebu yetu kama ninyi – walio na heshima ya kufunza ukweli.”
Kwa hivyo, njia iliyosahihi, ni kuweka wazi kuanzia mwanzo kuwa tuna roho sahihi – wapole, wenye roho ya unyenyekevu ya Mwalimu.
Mungu anaturuhusu kuona vitu katika Neno lake, na ni wakati mwafaka kwake kuwasha taa. Nuru ionekane. Picha ilikuwepo tangu hapo, lakini mawingu na giza vilifanya ionekane hafifu hivi kwamba tulikosa kuona urembo wake. Sasa nuru yazuka, kama vile malenga alivyoelezea.
“Vitu vya ajabu chuoni twaona.”
Badala ya kujitapa kwa kiburi, hekima yatuelekeza tusiuamini ubinafsi, tukikumbuka udhaifu wake na kutokamilika, na kwa mujibu wa heshima kubwa kwa Mungu na kumtegemea ambayo zaidi na kitu kingine chochote itatuimarisha na kutuwezesha kuondoka kwenye uovu wa hali yetu ya kuanguka.
Kwa kweli si jambo rahisi kuenenda katika njia ya unyenyekevu, kuendelea kuchunguza ya binadamu, na kuweka sadaka juu ya madhabahu mpaka imetumiwa kikamilifu. Lakini hivyo ni kwamba sisi tuutimize wokovu wetu wenyewe kwa kuogopa na kutetemeka, la sivyo tutakosa tuzo iliyoahidiwa kwa waaminifu wanaoshinda na wanaofuata kwa makini nyayo za Mtangulizi wetu mbarikiwa, ambaye alikuwa mpole na mwenye moyo wa unyenyekevu – Wafilipi 2:8,12
Tunapokuwa wanyenyekevu na waaminifu ndipo Bwana hutufanya vyombo vyake vilivyochaguliwa ili tulichukue jina lake kwa wengine. Kwa hiyo, tulishatengwa na kujazwa Roho Yake, twaweza kutenda, tukiwa na nguvu katika Bwana wa majeshi na nguvu zake kuu hufanya huduma ya mashujaa kuwa kama askari wa msalaba.