WAKILI DHALIMU
The Unjust Steward R5436
WAKILI DHALIMU
LUKA 16: 1 – 13
“Aliye mwaminifu katika lililo dogo kabisa huwa mwaminifu katika lilio kubwa pia: na aliye dhalimu katika lililo dogo kabisa huwa dhalimu katika lililo kubwa pia” –M:10.
Kwa kuwa mafarisayo ndio walikuwa wakiongoza katika kuunga mkono sheria, yesu alilenga mifano yake mingi kinyume chao huku kwa kulinganisha , alipuuzilia mbali wayahudi wasio wa kidini – yaani masadukayo , ambao hawakukiri imani. Funzo la leo linaambatana na hii. Mfano hii ilitolewa kama kemeo kwa roho wa mafarisayo ambao waliwekea wengine mizigo mizito, lakini wao wenyewe wakaihepa huku wakijifanya watiifu sana kwa sheria.
Katika nyakati za kale sana kupita sasa, ilikuwa tabia ya watu matajiri kuchagua mawakili. Wakili kama huyo alikuwa na utawala yote ju ya mali ya bwana wake kama vile bwana mwenyewe; alikuwa na uwezo kama ya mkubwa. Baadhi ya hao mawakili walikuwa waminifu; wengine wabadhirifu. Yule aliyetajwa katika mfano wa bwana wetu alikuwa kwenye fujo tena adimu. Bwana wake alikuwa ameamua kuondoa huduma zake na akawa amemwambia apeane hazina zake.
Katika vitabu zake kulikuwa na wenye deni ambao ilikuwa dhahiri kwamba waliachwa bila nafasi ya kuweza kufikiria wajibu wao. Huyo wakili alisema kwamba angepunguza hayo maddeni ili huenda wenye deni waweze kulipa kulipa kabla ya yeye kupeana ofisi yake kwa mridhi wake. Alitenda hivyo. Aliyekuwa na deni la vipimo mia moja vya mafuta aliambiwa angeweza punguza deni lake hadi hamsini. Mwengine aliyedaiwa makanda mia moja ya ngano aliambiwa apunguze asilimia ishirini. Akaendelea hivo na orodha. Jinsi hiyo ya kutumia mamlaka yake ilimfanya awe rafiki miongoni mwa wale aliowapa kibali; bwana wake naye akamsifu na kumpongeza kwa hekima aliyo onyesha.
Kutumia huo mfano, Yesu kwa jinsi vile alikashifu mafarisayo kwa kuchukua mkondo tofauti. Alikuwa ametangaza kuwa waandishi na mafarisayo walikaa katika kiti cha Musa kama watafsiri wa sheria za Musa, na kwamba walikuwa wamefuata njia ya huyo wakili. Wangejifanya kuwa marafiki wa watu maskini na wenye dhambi kwa kujaribu kupunguza uovu wao, na kuwwahimiza wafanye wawezavyo kutimiza matakwa ya sheria. Badala yake waliweka mzigo kwa watu na kuwakatisha jamaa.
Haya yote kwa upande wao ilikua ni unafiki; kwa kua hawangesaidia maana walijua wao wenyewe hawangeweza kutimiza matakwa ya sheria, ambayo ni kipimo kamili cha uwezo, wa mtu mkamilifu. Nia yao nzuri ingefaa iwe kufikiri uovu wao wenyewe, kujitahidi kutenda mema, kumsihi mungu rehema na kufundisha watu pia kutenda hivyo. Kutenda hivo kungewafanya wawe tayari kupokelewa katika kibali cha injili mwishoni mwa dahari. Kama ilivyokuwa kawaida ya unafiki wao, walikuwa wakijizuilia kufanyika wanafunzi wa yesu na kutafuta neema na kusamehewa dhambi. Walikua pia wanawazuia wengine kua wafuasi kwa kudai kwamba ilikua inawezekana kupata kibali kupitia kuhifadhi sheria.
KUTUMA MFANO
“ Yesu akawaambia wanafunzi wake , jifanyieni rafiki kwa mali ya udhalimu ili itakapokosekana – Mwisho wa uwakili wenu katika kifo- Matokeo ya wema wenu isababishe nyinyi mkubalike, katika ufufuo, kuingia katika makao ya milele”.
Kuna nafasi ya mabishano kuelekea mafundisho ya mfano huu, lakini kwetu sisi inaonekana wazi kwamba yesu alimaanisha kwamba hekima ya wakili dhalimu inafaa kiugwa na wanafunzi wake katika kushiriki na mamoni, matajiri wa maisha ya sasa.
Tangu wakati watu wa mungu wanajipeana kwa Mungu, Wanapeana pia haki yao na nia yao ya ulimwengu huu; Umenunuliwa kwa gharama; kwa hivyo mtukuze Mungu. “ Tuma yote uliyo nayo kwa nguvu kwa ajili ya utumishi w kitaua”.
Hawa mawakili wa rehema za Mungu wa kibali cha kutumia vitu vya dunia kujenga mahitaji yao ya kiroho; hawatahesabiwa dhalimu, kwa kuwa wanatumia fursa zao za kidunia kujenga mahitaji ya kimbingu. Kwa upande mwingine hii itahesabiwa kwao kama uwakili wa haki; na kupatikana waaminifu katika kutumia vitu vya ulimwengu katika utumishi wa Mungu, wanaweza dhaminiwa na mambo makuu ya usoni.
Watapokelewa katika makao ya milele, kupewa kushiriki na Masihi katika ufalme wake wa utukufu.
Watadhaminiwa na kibali chote cha Mungu juu wa wanadamu wote. Ukarimu wao katika hizi nyakati, uhiari wa kutoa dhabibu, itakua msingi wa kufuata kukubalika kwa kitaua na utukufu.
Kutokua mwaminifu nyakati za sasa na kuheshimu vitu zilizopungukiwa na udhamana inaweza onyesha kutokua mwaminifu katika mambo makuu yajayo. Yeyote atakayejipea vitu anazosimamia bila haki, hawezi dhaminiwa na mambo makuu ya usoni; na yeyote anayetoa dhabibu anaonyesha uaminifu wake na ukweli kwa Mungu, na kwao mambo makuu yatapeanwa. Je Mungu angeweza kudhamini watu wasio waaminifu na wachoyo, na wenye tamaa mbaya kwa mambo ya utajiri wake wa usoni? Hakika La! Hawezi!
Yesu nauliza “ikiwa haujakuwa mwaminifu kwa mali ya wengine, nani atakupea iliyo yako mwenyewe?”
Kwa wafuasi wa Yesu, mambo yote ya hizi nyakati za sasa ni za Mungu”- Mambo ya nyakati za sasa ni za Mungu. Kwa sababu tumeziweka. Wakfu. Vitu za Maisha ya usoni ni zetu. Kwa sababu Mungu ametuahidi. Lakini kuna kanuni: kama uaminifu wetu na ukweli wetu. Ikiwa sisi sio waaminifu katika kushughulikia mambo ambayo tumetolea wakfu kwa mungu, hawezi akatupea zile vitu alizosema zitakua zetu kikanuni. Kwa hivo ikiwa tutatumia vibaya na kuharibu uwakilishi wetu kwa kutumia hizo fursa kimakosa. Je tutatarajia Mungu apeane vitu alizoahidi kwa walio waaminfu
KUTUMIKIA MABWANA WAWILI
Kuna nguvu mbili zinazovutana; moja ovu na ingine njema. Hizi zinajulikana kwa majina nan i tofauti sana. Mungu ni bwana mwema; Shetani ni bwana muovu; lakini wote wanao wawakilishi. Kwa hivyo Mungu, roho wake na mafundisho yake, yanawakilishwa na neon upendo; ilhali shetani na njia zake huwakilishwa kwa uchoyo, tama mbaya na mamoni. Kupitia kuanguka kwa binadamu, ulimwengu wote umepoteza roho wa Mungu na umekua chini ya utawala wa shetani kwa miaka. Wote wamefanyika ovu kwa wingi au uchache. Roho ya uchoyo, tamaa mbaya na uovu ikisababisha udhalimu kwa kumjulisha, imetutawala kiasi kwamba hata baada ya kuona mkondo mbaya, ni vigumu sana kuharibu nguvu zake. “ Hatuwezi fanya vitu ambavyo tungekua tumefanya.
Lakini haya ndio mapendekezo ya injili: Mungu ananatamani kuona nafsi aminifu ili kujiunga na Yesu katika kupeana baraka zake. Anazawadi tuzo hii kuu ya ufalme kwa wale watakao onesha kuwa wana Roho wa haki. Tuzo hii ni ya dhamana sana. Hakuna jambo itakaloweza kulingana nayo. Yeyote ambaye anakubali injili kwa hekima anaziacha dhambi na uovu na mambo yote ya matendo ya kimwili na yanayohusu shetani na anaweka uso wake kuelekea kwa Mungu, upendo na haki.
Lakini haitashi kwamba ataingia katika agano kuacha ulimwengu na kuzifuata nyayo za Yesu. Haitoshi kwamba Mungu anakubali agano na kumtoa Roho wake mtakatifu. Zaidi ya hii inahitajika. Lazima aonyeshe kuwa hanapendelei tu mema kuliko maovu, lakini aonyeshe kwamba ako na uhiari wa kuteseka kupoteza mambo yote ili awe upande wa wema, upande wa Mungu.
Kisha huja majaribu. Mtu anatafuta kumtumikia Mungu na kupata thawabu ya utukufu, heshima na kutobatilika katika ufalme na Yesu: lakini anapata mazoea kwa mwili wake kutafuta na kufurahia mambo ya mamoni na uovu. Hii huleta vita kubwa. Na mmoja au mwingine lazima ashinde. Kwa kuongezea katika kukua ndani ya neema, ufahamu na upendo, kiumbe mpya katika Kristo lazima ajijaze na himizo na ahadi za bibilia la sivyo atakata tama na aache kabisa kupinga ulimwengu, umwili na shetani.
Bwana ameahidi neema ya kutosha wakati wote wa uhitaji, kwa waaminifu(Waebrania 4:16). Ana tuambia kwamba anajua sisi ni mavumbi. Anakumbuka umbo wetu (Zaburi 103:14), kwamba hatuwezi fanya ambayo tungependa kufany. Lakini kwa wakati huo huo anatuhitaji tutende yote tuwezavyo, akituhakikishia kwa hayo yote neema yake itatutosha; hio ni kusema, kwa hayo yote uweza wake utatimilisha udhaifu (2 Wakorintho 12:9)
Katika mafunzo yetu, Yesu anatuonya mwanzo kwamba chaguo letu lafaa kua la milele; kwamba fikra kuwa twaweza mtumkia Mungu na mamoni kwa wakati mmoja ni makosa (Mathayo 6:24) Luka 16:13). Kwa jinsi vile tutakosa kua waaminifu kwa mmoja ndivyo hivyo tutakua waaminifu kwa wengine. Kwa hivyo ni juu yetu kuchagua kumtumikia Mungu tukihesabu ni tunuku kubwa sana kwetu na thawabu kubwa zaidi ya milele.
Hata hivo, mengi yataegemea katika kipimo cha imani yetu. Tukiwa na imani katika Mung, ahadi ya thawabu yake kuu na ahadi ya mwokozi kutupea neema yake na msaada wakati wa uhitaj, itawezekana kwetu kupigana vita vizuri na kupata taji ambayo Bwana ametuwekea na wote wanaompenda kabisa (Timotheo Wa Pili 4:7-8).